丁支同嫲嫲一齊住。
Tingi aliishi na bibi yake.
丁支成日同嫲嫲一齊睇住班牛。
Alizoea kuchunga ng’ombe na bibi yake.
有一日,條村度嚟咗班士兵。
Siku moja wanajeshi walikuja.
丁支同嫲嫲逃離咗條村,匿埋咗。
Tingi na bibi yake walikimbia na kujificha.
佢哋匿埋喺樹叢度,一直到天黑。
Walijificha kichakani hadi usiku.
嫲嫲幫丁支𢫏住啲樹葉俾佢匿埋喺底下。
Bibi alimficha Tingi chini ya majani.
有個士兵踩到丁支藏身嘅樹葉上面,但係丁支都冇出聲。
Mwanajeshi mmoja alimkanyaga, lakini akanyamaza kimya.
丁支同嫲嫲等到周圍安全先走咗出嚟。
Wanajeshi walipoondoka Tingi na bibi yake wakajitokeza.
佢哋靜雞雞爬返屋企。
Wakajikongoja kimya kimya kurudi nyumbani.