Seine Hacke war zu kurz.
Jembe lake lilikuwa fupi mno.
Sein Türrahmen war zu niedrig.
Mlango wake ulikuwa chini mno.
Sein Bett war zu kurz.
Kitanda chake kilikuwa kifupi mno.
Sein Fahrrad war zu klein.
Baisikeli yake ilikuwa fupi sana.
Dieser Mann war zu groß!
Mtu huyu alikuwa mrefu zaidi!
Er bastelte einen sehr langen Griff für die Hacke.
Alitengeneza mpini wa jembe mrefu sana.
Er stellte sehr hohe Türrahmen her.
Alitengeneza fremu ndefu za milango.
Er stellte ein sehr langes Bett her.
Alitengeneza kitanda kirefu sana.
Er kaufte ein sehr großes Fahrrad.
Akanunua baisikeli iliyokuwa ndefu mno.
Er saß auf einem sehr hohen Stuhl. Er aß mit einer sehr langen Gabel.
Aliketi juu ya kiti kilichokuwa juu sana. Alikula kwa kutumia uma iliyokuwa ndefu mno.
Er verließ sein Haus und lebte in einem großen Wald. Er lebte viele Jahre lang.
Aliacha nyumba yake na kuishi katika msitu mkubwa. Aliishi kwa miaka mingi.