Back to stories list
Zama ni mkubwa!
Zama is great!
zama ni mkuɓwa
Michael Oguttu
Vusi Malindi
Matteo E. Mwita
Lauwo George
![Autoplay story](https://dohliam.github.io/elegant-circles/svg/play.svg)
Mdogo wangu anachelewa kuamka. Mimi naamka mapema kwa sababu mimi ni mkubwa!
My little brother sleeps
very late.
I wake early, because I
am great!
mɗoɠo waᵑgu @anachelewa kuamka mimi naamka mapema kwa saɓaɓu mimi ni mkuɓwa
Mimi ndiye ninayeruhusu jua kuingia ndani.
I am the one who lets in
the sun.
mimi ⁿɗije @ninayeruhusu ʄua kuiᵑgia ⁿɗani
“Wewe ni nyota wangu wa asubuhi,” anasema mama.
“You’re my morning
star,” says Ma.
wewe ni ɲota waᵑgu wa asuɓuhi anasema @mama
Naoga mwenyewe, sihitaji msaada.
I wash myself, I don’t
need any help.
@naoga mweɲewe @sihitaji msaaɗa
Naweza kustahimili maji ya baridi na sabuni ya bluu inayonukia.
I can cope with cold
water and blue smelly
soap.
naweza kustahimili maʄi ja ɓaɾiɗi na saɓuni ja ɓluu @inayonuka
Mama ananikumbusha, “Usisahau kupiga mswaki.” Namjibu, “Kamwe, sio mimi!”
Ma reminds, “Don’t
forget teeth.”
I reply, “Never, not
me!”
@mama @ananikumbusha usisahau kupiɠa mswaki @namjibu kamwe sio mimi
Baada ya kuoga, nawasalimu babu na shangazi, na kuwatakia siku njema.
After washing, I greet
Grandpa and Auntie,
and wish them a good
day.
ɓaaɗa ja kuoɠa nawasalimu ɓaɓu na ʃaᵑgazi na kuwatakia siku ⁿɗʒema
Najivisha nguo mwenyewe. “Mimi ni mkubwa sasa mama,” ninamwambia.
Then I dress myself,
“I’m big now Ma,” I say.
@najivisha ᵑguo mweɲewe mimi ni mkuɓwa sasa @mama @ninamwambia
Ninaweza kufunga vishikizo na kurekebisha viatu vyangu.
I can close my buttons
and buckle my shoes.
ninaweza kufuᵑga @vishikizo na kuɾekeɓiʃa viatu vjaᵑgu
Na ninahakikisha mdogo wangu anapata taarifa zote za shule.
And I make sure little
brother knows all the
school news.
na @ninahakikisha mɗoɠo waᵑgu anapata taaɾifa zote za ʃule
Darasani najitahidi sana katika kila kitu.
In class I do my best in
every way.
ɗaɾasani naʄitahiɗi sana katika kila kitu
Ninafanya hivi vitu vyote vizuri kila siku. Ila kitu ninachokipenda sana ni kucheza na kucheza.
I do all these good
things every day.
But the thing I like
most, is to play and
play!
ninafaɲa hivi vitu vjote vizuɾi kila siku ila kitu @ninachokipenda sana ni kutʃeza na kutʃeza
Written by: Michael Oguttu
Illustrated by: Vusi Malindi
Translated by: Matteo E. Mwita
Read by: Lauwo George