Download PDF
Back to stories list

Watoto wa nta Children of wax watoto wa nta

Written by Southern African Folktale

Illustrated by Wiehan de Jager

Translated by Mutugi Kamundi

Read by Lauwo George

Language Kiswahili

Level Level 2

Narrate full story

Autoplay story


Hapo zamani za kale, paliishi familia yenye furaha.

Once upon a time, there lived a happy family.

hapo zamani za @kale @paliishi familia jeɲe fuɾaha


Hawakugombana hata kidogo. Watoto waliwasaidia wazazi nyumbani na shambani.

They never fought with each other. They helped their parents at home and in the fields.

@hawakugombana hata kiɗoɠo watoto @waliwasaidia wazazi ɲuᵐɓani na ʃaᵐɓani


Lakini, walikatazwa kwenda karibu na moto.

But they were not allowed to go near a fire.

lakini @walikatazwa kweⁿɗa kaɾiɓu na moto


Walifanya kazi zao zote usiku. Hii ni kwa sababu walikuwa wameumbwa kwa nta.

They had to do all their work during the night. Because they were made of wax!

walifaɲa kazi zao zote usiku hii ni kwa saɓaɓu walikuwa wameuᵐɓwa kwa nta


Lakini, kijana mmoja alitamani kwenda nje wakati wa mchana.

But one of the boys longed to go out in the sunlight.

lakini kiʄana mmoʄa alitamani kweⁿɗa ⁿɗʒe wakati wa mtʃana


Siku moja tamaa ya kwenda nje ikazidi. Wenzake wakamwonya asiende juani. Lakini, hakusikia.

One day the longing was too strong. His brothers warned him…

siku moʄa tamaa ja kweⁿɗa ⁿɗʒe ikaziɗi weⁿzake @wakamwonya asieⁿɗe ʄuani lakini @hakusikia


Aliyeyuka kwa sababu joto lilikuwa kali.

But it was too late! He melted in the hot sun.

@aliyeyuka kwa saɓaɓu ʄoto lilikuwa kali


Watoto wa nta walihuzunika walipoona kaka yao akiyeyuka.

The wax children were so sad to see their brother melting away.

watoto wa nta @walihuzunika walipoona kaka jao @akiyeyuka


Wakapanga jambo fulani. Walichukua nta iliyoyeyuka wakatengeza ndege.

But they made a plan. They shaped the lump of melted wax into a bird.

@wakapanga ʄaᵐɓo fulani walitʃukua nta ilijojejuka @wakatengeza ⁿɗeɠe


Wakamweka ndege huyo juu ya mlima mrefu.

They took their bird brother up to a high mountain.

wakamweka ⁿɗeɠe hujo ʄuu ja mlima mɾefu


Jua lilipochomoza asubuhi, akapeperuka akiimba kwa furaha.

And as the sun rose, he flew away singing into the morning light.

ʄua lilipotʃomoza asuɓuhi @akapeperuka akiiᵐɓa kwa fuɾaha


Written by: Southern African Folktale
Illustrated by: Wiehan de Jager
Translated by: Mutugi Kamundi
Read by: Lauwo George
Language: Kiswahili
Level 2
Source: Children of wax from African Storybook
Creative Commons License
This work is licensed under a Creative Commons Attribution 3.0 International License.
Options
Back to stories list Download PDF