Download PDF
Back to stories list

Mbuzi, Mbwa na Ng’ombe Goat, Dog and Cow ᵐɓuzi ᵐɓwa na ŋoᵐɓe

Written by Fabian Wakholi

Illustrated by Marleen Visser, Ingrid Schechter

Translated by Brigid Simiyu

Read by Lauwo George

Language Kiswahili

Level Level 2

Narrate full story

Autoplay story


Mbuzi, Mbwa na Ng’ombe walikuwa marafiki wa karibu sana. Siku moja walisafiri kwa teksi.

Goat, Dog, and Cow were great friends. One day they went on a journey in a taxi.

ᵐɓuzi ᵐɓwa na ŋoᵐɓe walikuwa maɾafiki wa kaɾiɓu sana siku moʄa walisafiɾi kwa teksi


Walipofika mwisho wa safari yao, dereva aliwaomba walipe nauli zao. Ng’ombe alilipa nauli yake.

When they reached the end of their journey, the driver asked them to pay their fares. Cow paid her fare.

walipofika mwiʃo wa safaɾi jao ɗeɾeva aliwaoᵐɓa @walipe nauli zao ŋoᵐɓe @alilipa nauli jake


Mbwa alilipa zaidi kidogo kwa sababu hakuwa na pesa taslimu.

Dog paid a bit extra, because he did not have the correct money.

ᵐɓwa @alilipa zaiɗi kiɗoɠo kwa saɓaɓu hakuwa na pesa taslimu


Dereva alipokaribia kumpa Mbwa chenji yake, Mbuzi alitoroka bila kulipa chochote.

The driver was about to give Dog his change when Goat ran away without paying anything.

ɗeɾeva alipokaɾiɓia kumpa ᵐɓwa tʃeⁿɗʒi jake ᵐɓuzi @alitoroka ɓila kulipa tʃotʃote


Dereva alikasirika sana. Aliondoka bila kumrudishia Mbwa chenji yake.

The driver was very annoyed. He drove away without giving Dog his change.

ɗeɾeva alikasiɾika sana alioⁿɗoka ɓila @kumrudishia ᵐɓwa tʃeⁿɗʒi jake


Hiyo ndiyo sababu hadi leo Mbwa hukimbiza magari ili achungulie ndani kuona kama atampata dereva mwenye chenji yake.

That is why, even today, Dog runs towards a car to peep inside and find the driver who owes him his change.

hijo ⁿɗijo saɓaɓu haɗi leo ᵐɓwa hukiᵐɓiza maɠaɾi ili atʃuᵑgulie ⁿɗani kuona kama @atampata ɗeɾeva mweɲe tʃeⁿɗʒi jake


Mbuzi hukimbia anaposikia mlio wa gari. Anaogopa atakamatwa kwa kutolipa nauli.

Goat runs away from the sound of a car. She is afraid she will be arrested for not paying her fare.

ᵐɓuzi hukiᵐɓia anaposikia mlio wa ɠaɾi anaoɠopa @atakamatwa kwa @kutolipa nauli


Na Ng’ombe hababaiki gari likiwa linakuja. Ng’ombe huvuka barabara bila wasiwasi kwa sababu anajua alilipa nauli yake yote.

And Cow is not bothered when a car is coming. Cow takes her time crossing the road because she knows she paid her fare in full.

na ŋoᵐɓe haɓaɓaiki ɠaɾi likiwa @linakuja ŋoᵐɓe @huvuka ɓaɾaɓaɾa ɓila wasiwasi kwa saɓaɓu anaʄua @alilipa nauli jake jote


Written by: Fabian Wakholi
Illustrated by: Marleen Visser, Ingrid Schechter
Translated by: Brigid Simiyu
Read by: Lauwo George
Language: Kiswahili
Level 2
Source: Goat, Dog and Cow from African Storybook
Creative Commons License
This work is licensed under a Creative Commons Attribution 3.0 International License.
Options
Back to stories list Download PDF