Back to stories list
Uamuzi
Decision
uamuzi
Ursula Nafula
Vusi Malindi
Ursula Nafula
Lauwo George
Kijiji changu kilikuwa na matatizo mengi. Tulipanga foleni ndefu tukisubiri kuchota maji kutoka mfereji mmoja.
My village had many problems.
We made a long line to fetch water from one tap.
kiʄiʄi tʃaᵑgu kilikuwa na matatizo meᵑgi @tulipanga foleni ⁿɗefu @tukisubiri kutʃota maʄi kutoka mfeɾeʄi mmoʄa
Tulisubiri kupokea msaada wa chakula.
We waited for food donated by others.
@tulisubiri kupokea msaaɗa wa tʃakula
Tulifunga nyumba zetu mapema kwasababu ya wizi.
We locked our houses early because of thieves.
tulifuᵑga ɲuᵐɓa zetu mapema @kwasababu ja wizi
Watoto wengi waliacha shule.
Many children dropped out of school.
watoto weᵑgi waliatʃa ʃule
Wasichana wadogo walifanya kazi za nyumbani kwenye vijiji vingine.
Young girls worked as maids in other villages.
wasitʃana waɗoɠo walifaɲa kazi kama watumiʃi kweɲe viʄiʄi viᵑgine
Wavulana wadogo waliranda randa kijijini na wengine walifanya kazi kwenye mashamba ya watu.
Young boys roamed around the village while others worked on people’s farms.
wavulana waɗoɠo @waliranda ɾaⁿɗa kiʄiʄini na weᵑgine walifaɲa kazi kweɲe maʃaᵐɓa ja watu
Upepo ulipovuma, ulipeperusha karatasi chafu na kuzifikisha mitini na uani.
When the wind blew, waste paper hung on trees and fences.
upepo @ulipovuma @ulipeperusha kaɾatasi tʃafu na @kuzifikisha mitini na uani
Watu walikatwa na vipande vya chupa vilivyotupwa ovyo ovyo.
People were cut by broken glass that was thrown carelessly.
watu @walikatwa na vipaⁿɗe vja tʃupa @vilivyotupwa ovjo ovjo
Halafu siku moja, mfereji wa maji ulikauka na mitungi yetu ikawa mitupu.
Then one day, the tap dried up and our containers were empty.
halafu siku moʄa mfeɾeʄi wa maʄi @ulikauka na mituᵑgi jetu ikawa kawa tupu
Baba yangu alitembea nyumba hadi nyumba akiwaomba watu kuhudhuria mkutano wa kijiji.
My father walked from house to house asking people to attend a village meeting.
ɓaɓa jaᵑgu @alitembea kutoka ɲuᵐɓa haɗi ɲuᵐɓa @akiwaomba watu kuhuɗhuɾia mkutano wa kiʄiʄi
Watu walikusanyika chini ya mti mkubwa na kusikiliza.
People gathered under a big tree and listened.
watu @walikusanyika tʃini ja mti mkuɓwa na kusikiliza
Baba yangu alisimama na kusema, “Tunahitaji kusaidiana kutatua matatizo yetu.”
My father stood up and said, “We need to work together to solve our problems.”
ɓaɓa jaᵑgu alisimama na kusema tunahitaʄi kusaiɗiana kutatua matatizo jetu
Juma, mtoto wa miaka minane aliyekuwa amekaa kwenye tawi la mti, alisema kwa sauti, “Naweza kusaidia na usafi.”
Eight-year-old Juma, sitting on a tree trunk shouted, “I can help with cleaning up.”
ʄuma mtoto wa miaka minane alijekuwa amekaa kweɲe tawi la mti alisema kwa sauti naweza kusaiɗia na usafi
Mwanamke mmoja alisema, “Sisi wanawake tunaweza kuungana na kulima.”
One woman said, “The women can join me to grow food.”
mwanamke mmoʄa alisema sisi wanawake tunaweza kuuᵑgana na kuoteʃa tʃakula
Mwanamume mwingine alisimama na kusema, “Wanaume watachimba kisima cha maji.”
Another man stood up and said, “The men will dig a well.”
mwanamume mwiᵑgine alisimama na kusema wanaume @watachimba kisima tʃa maʄi
Sote tulisema kwa sauti moja, “Lazima tubadilishe maisha yetu.” Tangu siku hiyo, tulifanya kazi pamoja kutatua shida zetu.
We all shouted with one voice, “We must change our lives.”
From that day we worked together to solve our problems.
sote tulisema kwa sauti moʄa lazima @tubadilishe maiʃa jetu taᵑgu siku hijo tulifaɲa kazi pamoʄa kutatua ʃiɗa zetu
Written by: Ursula Nafula
Illustrated by: Vusi Malindi
Translated by: Ursula Nafula
Read by: Lauwo George