Hapo zamani za kale, paliishi familia yenye furaha.
很久很久以前,有一家人快乐地生活在一起。
Hawakugombana hata kidogo. Watoto waliwasaidia wazazi nyumbani na shambani.
孩子们从来不打架,还帮助爸爸妈妈做家务,干农活。
Lakini, walikatazwa kwenda karibu na moto.
但是他们不能靠近火焰。
Walifanya kazi zao zote usiku. Hii ni kwa sababu walikuwa wameumbwa kwa nta.
没办法,他们只能在晚上工作,因为他们都是用蜡做的!
Lakini, kijana mmoja alitamani kwenda nje wakati wa mchana.
但是其中一个男孩非常想出门,他想走到太阳底下看看。
Siku moja tamaa ya kwenda nje ikazidi. Wenzake wakamwonya asiende juani. Lakini, hakusikia.
有一天,这种渴望太强烈了。虽然他的兄弟们警告过他……
Aliyeyuka kwa sababu joto lilikuwa kali.
但是太晚了!他在太阳底下融化了。
Watoto wa nta walihuzunika walipoona kaka yao akiyeyuka.
其他蜡做的孩子看到他们的兄弟融化消失了,非常伤心。
Wakapanga jambo fulani. Walichukua nta iliyoyeyuka wakatengeza ndege.
但是他们想出了一个好主意:他们把熔化的蜡块捏成了一只鸟。
Wakamweka ndege huyo juu ya mlima mrefu.
他们把变成鸟的兄弟带到了一座高山上。
Jua lilipochomoza asubuhi, akapeperuka akiimba kwa furaha.
太阳升起来了,他迎着晨光唱着歌,飞走了。