下载 PDF
返回故事列表

Andiswa Nyota wa Mpira wa Miguu 球星安迪斯瓦

作者 Eden Daniels

插图 Eden Daniels

译文 Matteo E. Mwita

配音 Lauwo George

语言 斯瓦希里语

级别 2级

将整故事念出来

播放速度

自动念故事


Andiswa alikuwa anawaangalia wavulana wakicheza mpira wa miguu. Alitamani kujiunga nao. Akamwomba kocha kufanya nao mazoezi.

安迪斯瓦喜欢看男孩子们踢足球,她多么希望自己也能加入他们啊!她跑去问教练,自己能不能跟男孩们一起训练。


Kocha akaweka mikono kiunoni. “Kwenye shule hii, ni wavulana pekee wanaoruhusiwa kucheza mpira wa miguu,” alisema.

教练两手叉着腰,摇了摇头说:“在这个学校,只有男孩们能踢足球。”


Wavulana walimwambia aende kucheza mpira wa wavu. Walisema mpira wa wavu ni kwa ajili ya wasichana na mpira wa miguu ni kwa wavulana. Andiswa alijisikia vibaya.

男孩们让安迪斯瓦去玩投球。他们觉得,女孩们应该玩儿投球,足球是男孩们的运动。安迪斯瓦很沮丧。


Siku iliyofuata, shule yao ilikuwa na mashindano makubwa ya mpira wa miguu. Kocha alikuwa na wasiwasi kwa kuwa mchezaji wake wa kutegemewa alikuwa mgonjwa na asingecheza.

第二天,学校里要举行一场盛大的足球比赛。教练有点儿担心,因为队里最棒的球员生病了,没法上场。


Andiswa alimwendea kocha na kumuomba kumruhusu acheze. Kocha hakujua afanye nini. Akaamua kumruhusu Andiswe ajiunge na timu.

安迪斯瓦跑到教练那里,求他让自己替补上场。教练犹豫不决,最后他决定让安迪斯瓦试一试。


Mchezo ulikuwa mgumu. Hakuna timu yoyote iliyokuwa imefunga goli hadi muda wa mapumziko.

比赛很激烈,半场结束后,两队都没有进球。


Wakati wa kipindi cha pili kijana mmoja alimpatia Andiswa mpira. Akakimbia kwa kasi sana kuelekea golini. Akaupiga mpira kwa nguvu na akafunga goli.

比赛的下半场,一个男孩把球传给安迪斯瓦,安迪斯瓦飞快地朝球门跑去,用力一踢,球进了!


Umati ukashangilia kwa vifijo na furaha. Kuanzia siku hiyo, wasichana waliruhusiwa kucheza mpira wa miguu kwenye timu ya shule.

人群沸腾了!从那天开始,女孩们也可以在学校踢足球了。


作者: Eden Daniels
插图: Eden Daniels
译文: Matteo E. Mwita
配音: Lauwo George
语言: 斯瓦希里语
级别: 2级
出处: 原文来自非洲故事书Andiswa Soccer Star
共享创意授权条款
本着作系采用共享创意 署名-非商业性 3.0 未本地化版本授权条款授权。
选项
返回故事列表 下载 PDF