Tom anabeba tenga la ndizi zilizoiva.
汤姆顶着一篮熟透的香蕉。
Tom anaenda sokoni kuuza ndizi.
汤姆去集市上卖香蕉。
Sokoni watu wananunua matunda.
很多人去集市上买水果。
Lakini hakuna anayenunua ndizi za Tom. Wanapenda kununua matunda kutoka kwa akina mama.
但是没有人去汤姆那儿,因为他们更喜欢去女人们那儿买。
“Kwenye jamii yetu, ni wanawake pekee ndio wanaouza matunda,” watu wanasema. “Ni mwanamume wa aina gani huyu?” watu wanahoji.
人们说:“在我们这儿,只有女人会去卖水果”。他们问:“什么男人会去卖水果啊?”
Lakini Tom hakati tamaa. Anaita, “Nunua ndizi zangu! Nunueni ndizi zangu tamu zilizoiva!”
但是汤姆没有放弃。他在集市上叫卖:“快来买我的香蕉!又大又甜的香蕉!”
Mwanamke mmoja anachukua kichane cha ndizi kutoka kwenye tenga. Anaziangalia ndizi kwa umakini.
有一个妇女从篮子里抓了一把香蕉,仔细地查看。
Watu wengine wanakuja kwenye kichanja. Wananunua ndizi za Tom na kuzila.
越来越多的人到汤姆的摊位前。他们买了汤姆的香蕉,吃得津津有味。
Mara, tenga linakuwa tupu. Tom anahesabu pesa alizopata.
不一会儿,汤姆的篮子就空了,他数了数自己卖香蕉赚到的钱。
Tom ananunua sabuni, sukari, na mkate. Anaweka vitu kwenye tenga lake.
汤姆用这些钱买了肥皂、糖和面包。他把这些东西放在他的篮子里。
Tom anajitwisha tenga kichwani na kwenda nyumbani.
汤姆把篮子稳稳当当地顶在头上,回家了。