Kijiji changu kilikuwa na matatizo mengi. Tulipanga foleni ndefu tukisubiri kuchota maji kutoka mfereji mmoja.
我的村庄面临很多问题。村里只有一个水龙头,我们每天都要排很长的队伍去接水。
Tulisubiri kupokea msaada wa chakula.
我们等着别人接济食物给我们吃。
Tulifunga nyumba zetu mapema kwasababu ya wizi.
每天晚上,我们因为害怕有小偷,所以都早早地锁上了门。
Watoto wengi waliacha shule.
中途辍学的孩子也不少。
Wasichana wadogo walifanya kazi za nyumbani kwenye vijiji vingine.
年轻的女孩被迫到别的村庄去做女佣。
Wavulana wadogo waliranda randa kijijini na wengine walifanya kazi kwenye mashamba ya watu.
年轻的男孩不是成天在村子里游荡,就是到别人的农场里打工。
Upepo ulipovuma, ulipeperusha karatasi chafu na kuzifikisha mitini na uani.
起风的时候,废纸到处乱飞,挂在树梢和篱笆上。
Watu walikatwa na vipande vya chupa vilivyotupwa ovyo ovyo.
碎玻璃扔得到处都是,很多人都被碎玻璃划伤了。
Halafu siku moja, mfereji wa maji ulikauka na mitungi yetu ikawa mitupu.
终于有一天,水龙头干涸了,人们接不到水了。
Baba yangu alitembea nyumba hadi nyumba akiwaomba watu kuhudhuria mkutano wa kijiji.
我的爸爸一家一家地劝说,召集村里的居民们开会。
Watu walikusanyika chini ya mti mkubwa na kusikiliza.
人们聚到一棵大树下,准备开会。
Baba yangu alisimama na kusema, “Tunahitaji kusaidiana kutatua matatizo yetu.”
我爸爸站起来,说:“我们必须团结起来,一起解决我们的问题。”
Juma, mtoto wa miaka minane aliyekuwa amekaa kwenye tawi la mti, alisema kwa sauti, “Naweza kusaidia na usafi.”
八岁的珠玛坐在树干上,大声说:“我可以帮忙清理村庄。”
Mwanamke mmoja alisema, “Sisi wanawake tunaweza kuungana na kulima.”
一个女人站起来说:“我可以找一些妇女,一起种庄稼。”
Mwanamume mwingine alisimama na kusema, “Wanaume watachimba kisima cha maji.”
又有一个男人站起来说:“男人们可以帮着打井。”
Sote tulisema kwa sauti moja, “Lazima tubadilishe maisha yetu.” Tangu siku hiyo, tulifanya kazi pamoja kutatua shida zetu.
我们异口同声地说:“我们必须改变我们的生活。”从那天开始,大伙儿都齐心协力,解决问题。