Kituo kidogo cha mabasi kijijini mwetu kilijaa shughuli za watu na mabasi. mabasi mengi yalikuwa yamejaa mizigo. Chini, palikuwa na mizigo zaidi ya kupakia. Makondakta walikuwa wanataja majina ya sehemu mabasi yalikokuwa yanaelekea.
我聽到售票員叫「入城啦!入城啦!向西行!」呢架就係我要乘坐嘅大巴。
“Mjini! Mjini! Magharibi!” Nilisikia kondakta akiita kwa sauti. Lile ndilo basi nililohitaji kupanda.
Basi la kwenda mjini lilikaribia kujaa, lakini watu wengine walikuwa wanasukumana kupanda. Baadhi yao walipakia mizigo chini ya basi. Wengine waliiweka katika sehemu ya juu.
Nilijipenyeza ndani na kukaa karibu na dirisha. Mtu aliyeketi karibu nami alishika mfuko wa plastiki wa kijani kibichi. Alivaa viatu vilivyochakaa, koti kuukuu na alionekana kuwa na wasiwasi.
我望向窗外,先至意識到要離開培育我成人嘅村莊,要去大城市喇!
Niliangalia nje na kutambua kwamba nilikuwa naondoka kijijini kwangu, mahali ambapo nililelewa. Nilikuwa naenda katika mji mkubwa.
Upakiaji mizigo ulikamilika na abiria wakawa wameketi. Wachuuzi walizidi kusukumana kutaka kuingia ndani ya basi ili wauze bidhaa zao. Kila mmoja alitaja kwa sauti majina ya bidhaa alizokuwa anauza. Maneno yao yalinifurahisha.
有啲乘客買咗飲品,而有啲就買咗零食,仲即刻拆開嚟噍添。我呢啲冇錢嘅人就淨係可以睇住佢哋食。
Baadhi ya abiria walinunua vinywaji. Wengine wakanunua vitafunwa vidogo na kuanza kutafuna. Wasiokuwa na fedha, kama mimi, walitazama tu.
司機㩒咗幾次喇叭,要出發囉。售票員大聲嗌,叫啲小販快啲落車。
Shughuli hizi zilikatizwa kwa mlio wa honi ya basi, ishara kwamba tulikuwa tayari kuondoka. Kondakta aliwataka wachuuzi kuondoka ndani ya basi.
班小販推推㧬㧬噉落車,有啲仲忙住找錢俾人,而有啲就想把握最後一分鐘做生意。
Wachuuzi walisukumana huku wakitafuta njia ya kushuka. Wengine waliwarudishia wasafiri chenji zao. Wengine walifanya juhudi za mwisho kuuza bidhaa zao.
大巴慢慢離開咗車站,我望住窗外,唔知道今後會唔會有機會返嚟喇。
Basi lilipoondoka kituoni, nilichungulia dirishani. Nilijiuliza endapo ningerudi na kwenda kijijini kwangu tena.
旅程漸漸展開,車入面慢慢熱起上嚟,我瞇埋雙眼想瞌一陣。
Safari ilipoendelea, joto lilikuwa jingi ndani ya basi. Niliyafumba macho yangu nikinuia kulala.
但係我嘅思緒飄咗返屋企。我媽咪安唔安全呀?我養嘅兔仔賣唔賣到錢呀?我細佬記唔記得幫小樹苗淋水呀?
Lakini mawazo yangu yalirejea nyumbani. Je, mamangu atakuwa salama? Je, sungura wangu wataleta hela zozote? Je, ndugu yangu atakumbuka kunyunyizia maji miche ya miti yangu?
喺路上,我努力記住我叔叔住喺城市度嘅地址。我一路迷迷糊糊噉講住個地址,一路瞓著咗。
Njiani, nilikariri jina la mahali mjomba wangu alipoishi kwenye mji mkubwa. Nilikuwa bado nafikiria wakati nilipopatwa na usingizi.
過咗九個鐘,我被售票員嘅叫聲嘈醒,佢喺度嗌要坐車返條村嘅乘客。我拎返我個袋,跳咗落車。
Baada ya saa tisa, niliamshwa kwa kelele za kuita abiria waliokwenda katika kijiji changu. Nilichukuwa mfuko wangu mdogo na kuruka nje ya basi.
回程嘅大巴好快就坐滿晒,好快佢就會開返去東邊嘅村莊喇。對我嚟講,而家最緊要嘅就係要搵我叔叔間屋。
Basi la kurudi lilikuwa linajaa upesi. Muda mfupi baadaye, lingeanza safari ya kwenda mashariki. Jambo la maana kwangu wakati huo lilikuwa kuanza kutafuta nyumba ya mjomba wangu.