Kuku na Jongoo walikuwa marafiki. Ila walikuwa wanashindana kila mara. Siku moja wakaamua kucheza mpira wa miguu ili waweze kubaini nani alikuwa mchezaji bora zaidi.
Wakaenda uwanjani na wakaanza kucheza. Kuku alikuwa na kasi ila Jongoo alikuwa na kasi zaidi. Kuku alipiga mpira mbali, ila Jongoo alipiga mbali zaidi. Kuku akaanza kupandwa na hasira.
Kuku alipokuwa anarudi nyumbani alikutana na Mama yake Jongoo. Mama Jongoo akamuuliza, “Umemwona mwanangu?” Kuku hakujibu kitu. Mama Jongoo akapatwa na wasiwasi.
Mama Jongoo akasikia sauti kwa mbali. “Nisaidie mama!” ile sauti ililia. Mama Jongoo akaangalia huku na kule na kusikiliza kwa makini. Sauti ilitokea tumboni mwa kuku.
千足蟲媽咪大叫道:「快啲用你嘅神力!」千足蟲會產生一種好難聞嘅味道,會令到雞作嘔。
Mama Jongoo alipiga kelele, “Tumia nguvu yako ya kipekee mwanangu!” Majongoo wanaweza kutoa harufu mbaya na ladha ya ajabu. Kuku akaanza kujisikia mgonjwa.
雞打咗思噎,咕嚕咕嚕想作嘔,又打乞嗤又咳。千足蟲太嘔心喇!
Kuku akabeuwa. Akameza mate na kutema. Halafu akapiga chafya na kukohoa. Akakohoa tena. Jongoo alimfanya ajisikie vibaya.
雞不停噉咳,直到胃入面條千足蟲咳咗出嚟為止。千足蟲媽咪同個仔急住爬上樹,匿埋咗。
Kuku alikohoa, hadi akamtema jongoo aliyekuwa tumboni mwake. Mama Jongoo na mwanaye wakakwea mti kujificha.