Akawa kila siku anampikia, anamfulia na kumfagilia mbwa. Siku moja mbwa akasema, “Nozibele, leo naenda kuwatembelea rafiki zangu. Fagia nyumba, pika chakula na osha vitu vyangu kabla sijarudi.”

Mara baada tu ya mbwa kuondoka, Nozibele akanyofoa nywele tatu kutoka kwenye kichwa chake. Akaweka unywele mmoja chini ya kitanda, mmoja nyuma ya mlango, na mwingine akauweka kwenye uzio wa nyumba. Halafu, akakimbia kuelekea nyumbani kwa nguvu zote.

Mbwa aliporudi akaanza kumtafuta Nozibele. “Nozibele, uko wapi?” akapiga kelele. “Niko hapa, chini ya kitanda,” unywele wa kwanza ukajibu. “Nipo hapa nyuma ya mlango,” unywele wa pili ukajibu. “Niko hapa kwenye uzio,” unywele wa tatu ukajibu.

Mbwa akagundua kuwa Nozibele amemkimbia. Kwa hiyo akakimbia kuelekea kijijini. Kaka zake Nozibele walikuwa wakimsubiri na fimbo. Mbwa alipowaona akageuka na kukimbia, na hajawahi kuonekana tena.