Hapo zamani za kale, Kuku na Tai walikuwa marafiki. Waliishi kwa amani na ndege wengine. Hakuna kati yao aliyeweza kupaa.
Once upon a time, Hen and
Eagle were friends. They lived
in peace with all the other birds.
None of them could fly.
hapo zamani za @kale kuku na @tai walikuwa maɾafiki waliiʃi kwa amani na ⁿɗeɠe weᵑgine hakuna kati jao alijeweza kupaa
Kuna siku njaa ilitokea. Ikamlazimu Tai kutembea umbali mrefu kutafuta chakula. Alirudi akiwa amechoka sana. “Lazima kuwe na njia rahisi ya kusafiri!” Tai alisema.
One day, there was famine in
the land. Eagle had to walk very
far to find food. She came back
very tired.
“There must be an easier way
to travel!” said Eagle.
kuna siku ⁿɗʒaa ilitokea ikamlazimu @tai kuteᵐɓea uᵐɓali mɾefu kutafuta tʃakula aliɾuɗi akiwa @amechoka sana lazima kuwe na ⁿɗʒia ɾahisi ja kusafiɾi @tai alisema
Baada ya usingizi mnono wa usiku, Kuku alijiwa na wazo zuri sana. Akaanza kukusanya manyoya yaliyodondoka kutoka kwa ndege wenzao. “Tuyashonee haya manyoya juu ya manyoya yetu,” Kuku alisema. “Labda itaturahisishia kusafiri.”
After a good night’s sleep, Hen
had a brilliant idea. She began
collecting the fallen feathers
from all their bird friends.
“Let’s sew them together on top
of our own feathers,” she said.
“Perhaps that will make it easier
to travel.”
ɓaaɗa ja usiᵑgizi mnono wa usiku kuku @alijiwa na wazo zuɾi sana akaaⁿza kukusaɲa maɲoja @yaliyodondoka kutoka kwa ⁿɗeɠe weⁿzao @tuyashonee haja maɲoja ʄuu ja maɲoja jetu kuku alisema laɓɗa @itaturahisishia kusafiɾi
Tai pekee ndiye aliyekuwa na sindano kijijini, kwa hiyo akaanza kushona wa kwanza. Akajitengenezea mabawa mawili mazuri na akapaa juu ya kuku. Kuku aliazima sindano lakini akachoka kushona baada ya muda mfupi. Akaacha sindano kabatini na akaenda jikoni kuandaa chakula kwa ajili ya watoto wake.
Eagle was the only one in the
village with a needle, so she
started sewing first.
She made herself a pair of
beautiful wings and flew high
above Hen.
Hen borrowed the needle but
she soon got tired of sewing.
She left the needle on the
cupboard and went into the
kitchen to prepare food for her
children.
@tai pekee ⁿɗije alijekuwa na siⁿɗano kiʄiʄini kwa hijo akaaⁿza kuʃona wa kwaⁿza @akajitengenezea maɓawa mawili mazuɾi na @akapaa ʄuu ja kuku kuku @aliazima siⁿɗano lakini @akachoka kuʃona ɓaaɗa ja muɗa mfupi akaatʃa siⁿɗano @kabatini na akaeⁿɗa ʄikoni kuaⁿɗaa tʃakula kwa aʄili ja watoto @wake
Lakini ndege wengine walimwona Tai akipaa. Wakamwomba Kuku awaazime sindano ili nao wajishonee mabawa pia. Muda si mrefu ndege wakawa wamepaa na kuzagaa anga zima.
But the other birds had seen
Eagle flying away. They asked
Hen to lend them the needle to
make wings for themselves too.
Soon there were birds flying all
over the sky.
lakini ⁿɗeɠe weᵑgine walimwona @tai @akipaa wakamwoᵐɓa kuku @awaazime siⁿɗano ili nao @wajishonee maɓawa pia muɗa si mɾefu ⁿɗeɠe wakawa @wamepaa na @kuzagaa aᵑga zima
Ndege wa mwisho aliporudisha sindano aliyoazima, Kuku hakuwepo. Kwa hiyo watoto wake wakachukua sindano na wakaanza kuichezea. Walipochoka na mchezo wao, wakaiacha sindano kwenye mchanga.
When the last bird returned the
borrowed needle, Hen was not
there. So her children took the
needle and started playing with
it.
When they got tired of the
game, they left the needle in
the sand.
ⁿɗeɠe wa mwiʃo @aliporudisha siⁿɗano alijoazima kuku @hakuwepo kwa hijo watoto @wake wakatʃukua siⁿɗano na wakaaⁿza kuitʃezea @walipochoka na mtʃezo wao wakaiatʃa siⁿɗano kweɲe mtʃaᵑga
Baadaye jioni Tai akarudi. Akaomba sindano ili aweze kushona baadhi ya manyoya yaliyokuwa yameanza kulegea alipokuwa safarini. Akaangalia kwenye kabati. Akaangalia jikoni. Akaangalia uani. Ila sindano haikupatikana.
Later that afternoon, Eagle
returned. She asked for the
needle to fix some feathers that
had loosened on her journey.
Hen looked on the cupboard.
She looked in the kitchen. She
looked in the yard. But the
needle was nowhere to be
found.
ɓaaɗaje ʄioni @tai akaɾuɗi akaoᵐɓa siⁿɗano ili aweze kuʃona ɓaaɗhi ja maɲoja jalijokuwa jameaⁿza kuleɠea alipokuwa safaɾini @akaangalia kweɲe kaɓati @akaangalia ʄikoni @akaangalia uani ila siⁿɗano @haikupatikana
“Nipatie siku moja,” Kuku alimwomba Tai. “Halafu utaweza kushona bawa lako na kuruka tena kwenda kutafuta chakula.” “Siku moja tu,” alisema Tai. “Kama hutaipata sindano, itabidi unipe kimoja cha vifaranga vyako kama malipo.”
“Just give me a day,” Hen
begged Eagle. “Then you can
fix your wing and fly away to
get food again.”
“Just one more day,” said Eagle.
“If you can’t find the needle,
you’ll have to give me one of
your chicks as payment.”
nipatie siku moʄa kuku alimwoᵐɓa @tai halafu utaweza kuʃona ɓawa lako na kuɾuka tena kweⁿɗa kutafuta tʃakula siku moʄa tu alisema @tai kama @hutaipata siⁿɗano itaɓiɗi unipe kimoʄa tʃa vifaɾaᵑga vjako kama malipo
Tai aliporudi siku iliyofuata, alimkuta Kuku akichakura mchangani, ila hakukuwa na sindano. Kwa hiyo Tai alishuka kwa kasi na kukwapua kifaranga kimoja. Akaondoka nacho. Tangu hapo, kila Tai anapojitokeza humkuta Kuku akichakura kwenye mchanga akitafuta sindano.
When Eagle came the next day,
she found Hen scratching in the
sand, but no needle.
So Eagle flew down very fast
and caught one of the chicks.
She carried it away.
Forever after that, whenever
Eagle appears, she finds Hen
scratching in the sand for the
needle.
@tai alipoɾuɗi siku ilijofuata alimkuta kuku @akichakura mtʃaᵑgani ila hakukuwa na siⁿɗano kwa hijo @tai aliʃuka kwa kasi na @kukwapua kifaɾaᵑga kimoʄa akaoⁿɗoka @nacho taᵑgu hapo kila @tai @anapojitokeza @humkuta kuku @akichakura kweɲe mtʃaᵑga akitafuta siⁿɗano
Kila kivuli cha mabawa ya Tai kinapoonekana ardhini, Kuku huwatahadharisha vifaranga vyake. “Tokeni kwenye eneo la wazi.” Na wanajibu: “Sisi si wajinga. Tutakimbia.”
As the shadow of Eagle’s wing
falls on the ground, Hen warns
her chicks. “Get out of the bare
and dry land.”
And they respond:
“We are not fools. We will run.”
kila kivuli tʃa maɓawa ja @tai @kinapoonekana aɾɗhini kuku @huwatahadharisha vifaɾaᵑga vjake tokeni kweɲe eneo la wazi na @wanajibu: sisi si waʄiᵑga @tutakimbia