Download PDF
Back to stories list

Kuku na Jongoo Chicken and Millipede kuku na ʄoᵑgoo

Written by Winny Asara

Illustrated by Magriet Brink

Translated by Matteo E. Mwita

Read by Lauwo George

Language Kiswahili

Level Level 3

Narrate full story

Autoplay story


Kuku na Jongoo walikuwa marafiki. Ila walikuwa wanashindana kila mara. Siku moja wakaamua kucheza mpira wa miguu ili waweze kubaini nani alikuwa mchezaji bora zaidi.

Chicken and Millipede were friends. But they were always competing with each other. One day they decided to play football to see who the best player was.

kuku na ʄoᵑgoo walikuwa maɾafiki ila walikuwa @wanashindana kila maɾa siku moʄa wakaamua kutʃeza mpiɾa wa miɠuu ili waweze kuɓaini nani alikuwa mtʃezaʄi ɓoɾa zaiɗi


Wakaenda uwanjani na wakaanza kucheza. Kuku alikuwa na kasi ila Jongoo alikuwa na kasi zaidi. Kuku alipiga mpira mbali, ila Jongoo alipiga mbali zaidi. Kuku akaanza kupandwa na hasira.

They went to the football field and started their game. Chicken was fast, but Millipede was faster. Chicken kicked far, but Millipede kicked further. Chicken started to feel grumpy.

wakaeⁿɗa uwaⁿɗʒani na wakaaⁿza kutʃeza kuku alikuwa na kasi ila ʄoᵑgoo alikuwa na kasi zaiɗi kuku alipiɠa mpiɾa ᵐɓali ila ʄoᵑgoo alipiɠa ᵐɓali zaiɗi kuku akaaⁿza kupaⁿɗwa na hasiɾa


Wakaamua kupigiana penati. Jongoo akaenda golini. Kuku alifunga goli moja pekee. Ikawa zamu ya kuku kwenda golini.

They decided to play a penalty shoot-out. First Millipede was goal keeper. Chicken scored only one goal. Then it was the chicken’s turn to defend the goal.

wakaamua kupiɠiana @penati ʄoᵑgoo akaeⁿɗa @golini kuku alifuᵑga ɠoli moʄa pekee ikawa zamu ja kuku kweⁿɗa @golini


Jongoo alipiga mpira akafunga. Jongoo akapiga chenga akafunga. Jongoo akapiga kichwa akafunga. Jongoo akafunga magoli matano.

Millipede kicked the ball and scored. Millipede dribbled the ball and scored. Millipede headed the ball and scored. Millipede scored five goals.

ʄoᵑgoo alipiɠa mpiɾa akafuᵑga ʄoᵑgoo akapiɠa tʃeᵑga akafuᵑga ʄoᵑgoo akapiɠa kitʃwa akafuᵑga ʄoᵑgoo akafuᵑga maɠoli matano


Kuku akakasirika kwa kuwa amefungwa. Hakuwa mshindani mzuri. Jongoo akaanza kucheka kwa sababu rafiki yake alikuwa analalamika.

Chicken was furious that she lost. She was a very bad loser. Millipede started laughing because his friend was making such a fuss.

kuku akakasiɾika kwa kuwa amefuᵑgwa hakuwa mʃiⁿɗani mzuɾi ʄoᵑgoo akaaⁿza kutʃeka kwa saɓaɓu ɾafiki jake alikuwa @analalamika


Kuku alipatwa na hasira kiasi kwamba akafungua mdomo wake mkubwa na akammeza Jongoo.

Chicken was so angry that she opened her beak wide and swallowed the millipede.

kuku alipatwa na hasiɾa kiasi kwaᵐɓa akafuᵑgua mɗomo @wake mkuɓwa na @akammeza ʄoᵑgoo


Kuku alipokuwa anarudi nyumbani alikutana na Mama yake Jongoo. Mama Jongoo akamuuliza, “Umemwona mwanangu?” Kuku hakujibu kitu. Mama Jongoo akapatwa na wasiwasi.

As Chicken was walking home, she met Mother Millipede. Mother Millipede asked, “Have you seen my child?” Chicken didn’t say anything. Mother Millipede was worried.

kuku alipokuwa anaɾuɗi ɲuᵐɓani alikutana na @mama jake ʄoᵑgoo @mama ʄoᵑgoo @akamuuliza umemwona mwanaᵑgu kuku hakuʄiɓu kitu @mama ʄoᵑgoo @akapatwa na wasiwasi


Mama Jongoo akasikia sauti kwa mbali. “Nisaidie mama!” ile sauti ililia. Mama Jongoo akaangalia huku na kule na kusikiliza kwa makini. Sauti ilitokea tumboni mwa kuku.

Then Mother Millipede heard a tiny voice. “Help me mom!” cried the voice. Mother Millipede looked around and listened carefully. The voice came from inside the chicken.

@mama ʄoᵑgoo akasikia sauti kwa ᵐɓali nisaiɗie @mama ile sauti ililia @mama ʄoᵑgoo @akaangalia huku na kule na kusikiliza kwa makini sauti ilitokea tuᵐɓoni mwa kuku


Mama Jongoo alipiga kelele, “Tumia nguvu yako ya kipekee mwanangu!” Majongoo wanaweza kutoa harufu mbaya na ladha ya ajabu. Kuku akaanza kujisikia mgonjwa.

Mother Millipede shouted, “Use your special power my child!” Millipedes can make a bad smell and a terrible taste. Chicken began to feel ill.

@mama ʄoᵑgoo alipiɠa kelele tumia ᵑguvu jako ja kipekee mwanaᵑgu maʄoᵑgoo wanaweza kutoa haɾufu ᵐɓaja na laɗha ja aʄaɓu kuku akaaⁿza @kujisikia mɠoⁿɗʒwa


Kuku akabeuwa. Akameza mate na kutema. Halafu akapiga chafya na kukohoa. Akakohoa tena. Jongoo alimfanya ajisikie vibaya.

Chicken burped. Then she swallowed and spat. Then she sneezed and coughed. And coughed. The millipede was disgusting!

kuku @akabeuwa @akameza @mate na kutema halafu akapiɠa tʃafja na kukohoa @akakohoa tena ʄoᵑgoo alimfaɲa @ajisikie viɓaja


Kuku alikohoa, hadi akamtema jongoo aliyekuwa tumboni mwake. Mama Jongoo na mwanaye wakakwea mti kujificha.

Chicken coughed until she coughed out the millipede that was in her stomach. Mother Millipede and her child crawled up a tree to hide.

kuku @alikohoa haɗi @akamtema ʄoᵑgoo alijekuwa tuᵐɓoni mwake @mama ʄoᵑgoo na @mwanaye @wakakwea mti kuʄifitʃa


Tangu hapo, Kuku na Jongoo ni maadui.

From that time, chickens and millipedes were enemies.

taᵑgu hapo kuku na ʄoᵑgoo ni maaɗui


Written by: Winny Asara
Illustrated by: Magriet Brink
Translated by: Matteo E. Mwita
Read by: Lauwo George
Language: Kiswahili
Level 3
Source: Chicken and Millipede from African Storybook
Creative Commons License
This work is licensed under a Creative Commons Attribution 3.0 International License.
Options
Back to stories list Download PDF