Download PDF
Back to stories list

Wimbo wa Sakima Sakima's song wiᵐɓo wa @sakima

Written by Ursula Nafula

Illustrated by Peris Wachuka

Translated by Ursula Nafula

Read by Lauwo George

Language Kiswahili

Level Level 3

Narrate full story

Autoplay story


Sakima aliishi na wazazi wake na dada yake wa miaka minne. Waliishi katika shamba la mtu tajiri. Nyumba yao ya nyasi ilikuwa mwisho wa safu ya miti iliyopendeza.

Sakima lived with his parents and his four year old sister. They lived on a rich man’s land. Their grass-thatched hut was at the end of a row of trees.

@sakima aliiʃi na wazazi @wake na @dada jake wa miaka minne waliiʃi katika ʃaᵐɓa la mtu taʄiɾi ɲuᵐɓa jao ja ɲasi ilikuwa mwiʃo wa safu ja miti @iliyopendeza


Sakima alipokuwa na umri wa miaka mitatu, aliugua na kupoteza uwezo wa kuona. Hata hivyo, Sakima alikuwa mvulana mwenye kipaji.

When Sakima was three years old, he fell sick and lost his sight. Sakima was a talented boy.

@sakima alipokuwa na umɾi wa miaka mitatu aliuɠua na kupoteza uwezo wa kuona hata hivjo @sakima alikuwa ᵐvulana mweɲe kipaʄi


Sakima alitenda mambo mengi ambayo wavulana wengine wa umri wake hawakufanya. Kwa mfano, aliketi na watu wazima na kujadili mambo muhimu.

Sakima did many things that other six year old boys did not do. For example, he could sit with older members of the village and discuss important matters.

@sakima aliteⁿɗa @mambo meᵑgi aᵐɓajo wavulana weᵑgine wa umɾi @wake @hawakufanya kwa mfano @angeketi na watu wazima na kuʄaɗili @mambo muhimu


Wazazi wa Sakima walifanya kazi katika nyumba ya yule tajiri. Walitoka nyumbani asubuhi na mapema na kurudi jioni. Sakima aliachwa na dada yake.

The parents of Sakima worked at the rich man’s house. They left home early in the morning and returned late in the evening. Sakima was left with his little sister.

wazazi wa @sakima walifaɲa kazi katika ɲuᵐɓa ja jule taʄiɾi walitoka ɲuᵐɓani asuɓuhi na mapema na kuɾuɗi ʄioni @sakima @aliachwa na @dada jake


Sakima alipenda kuimba nyimbo. Siku moja mama yake alimuuliza, “Sakima, unajifunza nyimbo hizi kutoka wapi?”

Sakima loved to sing songs. One day his mother asked him, “Where do you learn these songs from, Sakima?”

@sakima alipeⁿɗa kuiᵐɓa ɲiᵐɓo siku moʄa @mama jake alimuuliza @sakima @unajifunza ɲiᵐɓo hizi kutoka wapi


Sakima alimjibu, “Nazisikia akilini mwangu kisha naziimba.”

Sakima answered, “They just come, mother. I hear them in my head and then I sing.”

@sakima alimʄiɓu @nazisikia akilini mwaᵑgu kiʃa @naziimba


Sakima alipenda kumwimbia mdogo wake hasa akihisi njaa. Dada yake alimsikiliza na kucheza.

Sakima liked to sing for his little sister, especially, if she felt hungry. His sister would listen to him singing his favourite song. She would sway to the soothing tune.

@sakima alipeⁿɗa kumwiᵐɓia mɗoɠo @wake hasa @akihisi ⁿɗʒaa @dada jake @alimsikiliza na kutʃeza


“Naomba uimbe tena na tena, Sakima,” mdogo wake alimsihi. Sakima alikubali na kuimba mara nyingine.

“Can you sing it again and again, Sakima,” his sister would beg him. Sakima would accept and sing it over and over again.

naoᵐɓa @uimbe tena na tena @sakima mɗoɠo @wake @alimsihi @sakima alikuɓali na kuiᵐɓa maɾa ɲiᵑgine


Jioni moja, wazazi wake waliporudi nyumbani, walikuwa kimya sana. Sakima alijua kwamba lazima kulikuwa na jambo baya.

One evening when his parents returned home, they were very quiet. Sakima knew that there was something wrong.

ʄioni moʄa wazazi @wake walipoɾuɗi ɲuᵐɓani walikuwa kimja sana @sakima aliʄua kwaᵐɓa lazima kulikuwa na ʄaᵐɓo ɓaja


“Kuna shida gani, mama, baba?” Sakima aliuliza. Sakima aligundua kwamba mwana wa tajiri wao alikuwa amepotea. Tajiri alihuzunika na kuwa na upweke mkubwa.

“What is wrong, mother, father?” Sakima asked. Sakima learned that the rich man’s son was missing. The man was very sad and lonely.

kuna ʃiɗa ɠani @mama ɓaɓa @sakima aliuliza @sakima aliɠuⁿɗua kwaᵐɓa mwana wa taʄiɾi wao alikuwa amepotea taʄiɾi alihuzunika na kuwa na upweke mkuɓwa


“Labda atafurahi tena nikimwimbia,” Sakima aliwaambia wazazi wake. Wazazi wake walidharau wazo lake. “Yeye ni tajiri sana. Wewe ni mvulana asiyeona. Unadhani wimbo wako utamsaidia?”

“I can sing for him. He might be happy again,” Sakima told his parents. But his parents dismissed him. “He is very rich. You are only a blind boy. Do you think your song will help him?”

laɓɗa atafuɾahi tena @nikimwimbia @sakima aliwaaᵐɓia wazazi @wake wazazi @wake @walidharau wazo @lake jeje ni taʄiɾi sana wewe ni ᵐvulana asijeona unaɗhani wiᵐɓo wako @utamsaidia


Hata hivyo, Sakima hakukata tamaa. Mdogo wake alimpa moyo. Alisema, “Nyimbo za Sakima hunituliza mimi nikiwa na njaa. Zitamtuliza tajiri vile vile.”

However, Sakima did not give up. His little sister supported him. She said, “Sakima’s songs soothe me when I am hungry. They will soothe the rich man too.”

hata hivjo @sakima @hakukata tamaa mɗoɠo @wake alimpa mojo alisema ɲiᵐɓo za @sakima @hunituliza mimi nikiwa na ⁿɗʒaa @zitamtuliza taʄiɾi @vile @vile


Siku iliyofuata, Sakima alimwomba mdogo wake amwongoze hadi kwenye nyumba ya tajiri.

The following day, Sakima asked his little sister to lead him to the rich man’s house.

siku ilijofuata @sakima alimwoᵐɓa mɗoɠo @wake amwoᵑgoze haɗi kweɲe ɲuᵐɓa ja taʄiɾi


Alisimama chini ya dirisha moja kubwa na kuanza kuimba wimbo wake alioupenda. Pole pole, kichwa cha tajiri kilionekana dirishani.

He stood below one big window and began to sing his favourite song. Slowly, the head of the rich man began to show through the big window.

alisimama tʃini ja ɗiɾiʃa moʄa kuɓwa na kuaⁿza kuiᵐɓa wiᵐɓo @wake alioupeⁿɗa pole pole kitʃwa tʃa taʄiɾi kilionekana ɗiɾiʃani


Wafanyakazi waliacha kazi zao. Wakasikiliza wimbo mzuri wa Sakima. Hata hivyo, mwanamume mmoja alisema, “Hakuna aliyefaulu kumtuliza bwana. Je, huyu mvulana asiyeona anafikiri atamtuliza?”

The workers stopped what they were doing. They listened to Sakima’s beautiful song. But one man said, “Nobody has been able to console the boss. Does this blind boy think he will console him?”

wafaɲakazi waliatʃa kazi zao wakasikiliza wiᵐɓo mzuɾi wa @sakima hata hivjo mwanamume mmoʄa alisema hakuna alijefaulu kumtuliza @bwana ʄe huju ᵐvulana asijeona anafikiɾi @atamtuliza


Sakima alipomaliza kuimba wimbo wake alianza kuondoka. Tajiri alitoka nje kwa haraka na kusema, “Tafadhali, imba tena.”

Sakima finished singing his song and turned to leave. But the rich man rushed out and said, “Please sing again.”

@sakima alipomaliza kuiᵐɓa wiᵐɓo @wake aliaⁿza kuoⁿɗoka taʄiɾi alitoka ⁿɗʒe kwa haɾaka na kusema tafaɗhali iᵐɓa tena


Wakati huo huo, watu wawili walikuja wakiwa wamembeba mtu kwenye machela. Walimkuta mwana wa tajiri akiwa amechapwa na kuachwa kando ya barabara.

At that very moment, two men came carrying someone on a stretcher. They had found the rich man’s son beaten up and left on the side of the road.

wakati huo huo watu wawili walikuʄa wakiwa @wamembeba mtu kweɲe matʃela walimkuta mwana wa taʄiɾi akiwa @amechapwa na kuatʃwa kaⁿɗo ja ɓaɾaɓaɾa


Tajiri alifurahi sana kumwona mwana wake tena. Alimzawadia Sakima kwa kumliwaza. Aliwapeleka mwanawe na Sakima hosipitali ili Sakima aweze kusaidiwa kuona tena.

The rich man was so happy to see his son again. He rewarded Sakima for consoling him. He took his son and Sakima to hospital so Sakima could regain his sight.

taʄiɾi alifuɾahi sana kumwona mwana @wake tena @alimzawadia @sakima kwa @kumliwaza @aliwapeleka mwanawe na @sakima @hosipitali ili @sakima aweze kusaiɗiwa kuona tena


Written by: Ursula Nafula
Illustrated by: Peris Wachuka
Translated by: Ursula Nafula
Read by: Lauwo George
Language: Kiswahili
Level 3
Source: Sakima's song from African Storybook
Creative Commons License
This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
Options
Back to stories list Download PDF