Download PDF
Back to stories list

Tingi na ng’ombe Tingi and the cows

Written by Ingrid Schechter

Illustrated by Ingrid Schechter

Translated by Matteo E. Mwita

Read by Lauwo George

Language Kiswahili

Level Level 2

Narrate full story

Reading speed

Autoplay story


Tingi aliishi na bibi yake.

Tingi lived with his grandmother.


Alizoea kuchunga ng’ombe na bibi yake.

He used to look after the cows with her.


Siku moja wanajeshi walikuja.

One day the soldiers came.


Wakawachukua ng’ombe.

They took the cows away.


Tingi na bibi yake walikimbia na kujificha.

Tingi and his grandmother ran away and hid.


Walijificha kichakani hadi usiku.

They hid in the bush until night.


Wanajeshi walirudi tena.

Then the soldiers came back.


Bibi alimficha Tingi chini ya majani.

Grandmother hid Tingi under the leaves.


Mwanajeshi mmoja alimkanyaga, lakini akanyamaza kimya.

One of the soldiers put his foot right on him, but he kept quiet.


Wanajeshi walipoondoka Tingi na bibi yake wakajitokeza.

When it was safe, Tingi and his grandmother came out.


Wakajikongoja kimya kimya kurudi nyumbani.

They crept home very quietly.


Written by: Ingrid Schechter
Illustrated by: Ingrid Schechter
Translated by: Matteo E. Mwita
Read by: Lauwo George
Language: Kiswahili
Level: Level 2
Source: Tingi and the Cows from African Storybook
Creative Commons License
This work is licensed under a Creative Commons Attribution 3.0 International License.
Options
Back to stories list Download PDF