Mdogo wangu anachelewa kuamka. Mimi naamka mapema kwa sababu mimi ni mkubwa!
My little brother sleeps very late. I wake early, because I am great!
Mimi ndiye ninayeruhusu jua kuingia ndani.
I am the one who lets in the sun.
“Wewe ni nyota wangu wa asubuhi,” anasema mama.
“You’re my morning star,” says Ma.
Naoga mwenyewe, sihitaji msaada.
I wash myself, I don’t need any help.
Naweza kustahimili maji ya baridi na sabuni ya bluu inayonukia.
I can cope with cold water and blue smelly soap.
Mama ananikumbusha, “Usisahau kupiga mswaki.” Namjibu, “Kamwe, sio mimi!”
Ma reminds, “Don’t forget teeth.” I reply, “Never, not me!”
Baada ya kuoga, nawasalimu babu na shangazi, na kuwatakia siku njema.
After washing, I greet Grandpa and Auntie, and wish them a good day.
Najivisha nguo mwenyewe. “Mimi ni mkubwa sasa mama,” ninamwambia.
Then I dress myself, “I’m big now Ma,” I say.
Ninaweza kufunga vishikizo na kurekebisha viatu vyangu.
I can close my buttons and buckle my shoes.
Na ninahakikisha mdogo wangu anapata taarifa zote za shule.
And I make sure little brother knows all the school news.
Darasani najitahidi sana katika kila kitu.
In class I do my best in every way.
Ninafanya hivi vitu vyote vizuri kila siku. Ila kitu ninachokipenda sana ni kucheza na kucheza.
I do all these good things every day. But the thing I like most, is to play and play!