Tingi vivia com a avó.
Tingi aliishi na bibi yake.
Tingi lived with his grandmother.
Ele costumava cuidar as vacas com ela.
Alizoea kuchunga ng’ombe na bibi yake.
He used to look after the cows with her.
Um dia, vieram os soldados.
Siku moja wanajeshi walikuja.
One day the soldiers came.
Tingi e a avó fugiram e esconderam-se.
Tingi na bibi yake walikimbia na kujificha.
Tingi and his grandmother ran away and hid.
Esconderam-se na mata até a noite.
Walijificha kichakani hadi usiku.
They hid in the bush until night.
Então, os soldados voltaram.
Wanajeshi walirudi tena.
Then the soldiers came back.
A avó escondeu Tingi em baixo das folhas.
Bibi alimficha Tingi chini ya majani.
Grandmother hid Tingi under the leaves.
Um dos soldados pisou em cima dele, mas Tingi manteve-se quieto.
Mwanajeshi mmoja alimkanyaga, lakini akanyamaza kimya.
One of the soldiers put his foot right on him, but he kept quiet.
Quando já era seguro, Tingi e a avó saíram do esconderijo.
Wanajeshi walipoondoka Tingi na bibi yake wakajitokeza.
When it was safe, Tingi and his grandmother came out.
Arrastaram-se silenciosamente até a casa.
Wakajikongoja kimya kimya kurudi nyumbani.
They crept home very quietly.