Es war einmal eine Henne und ein Adler, die Freunde waren. Sie lebten friedlich mit all den anderen Vögeln. Keiner von ihnen konnte fliegen.
Hapo zamani za kale, Kuku na Tai walikuwa marafiki. Waliishi kwa amani na ndege wengine. Hakuna kati yao aliyeweza kupaa.
Eines Tages überkam eine Hungersnot das Land. Adler musste sehr weit laufen, um Essen zu finden. Sie kam sehr müde zurück. „Es muss eine leichtere Art der Fortbewegung geben!“, rief Adler.
Kuna siku njaa ilitokea. Ikamlazimu Tai kutembea umbali mrefu kutafuta chakula. Alirudi akiwa amechoka sana. “Lazima kuwe na njia rahisi ya kusafiri!” Tai alisema.
Nach einer erholsamen Nacht hatte Henne eine großartige Idee. Sie machte sich daran, alle ausgefallenen Federn ihrer Vogelfreunde einzusammeln. „Lasst uns sie über unsere eigenen Federn nähen“, meinte sie. „Vielleicht wird so die Fortbewegung leichter.“
Baada ya usingizi mnono wa usiku, Kuku alijiwa na wazo zuri sana. Akaanza kukusanya manyoya yaliyodondoka kutoka kwa ndege wenzao. “Tuyashonee haya manyoya juu ya manyoya yetu,” Kuku alisema. “Labda itaturahisishia kusafiri.”
Adler war die einzige mit einer Nadel, also nähte sie zuerst. Sie nähte sich ein Paar wunderschöne Flügel und flog hoch über Henne. Henne borgte sich die Nadel, aber sie verlor schnell die Lust am Nähen. Sie ließ die Nadel auf dem Schrank und ging in die Küche, um Essen für ihre Kinder zu machen.
Tai pekee ndiye aliyekuwa na sindano kijijini, kwa hiyo akaanza kushona wa kwanza. Akajitengenezea mabawa mawili mazuri na akapaa juu ya kuku. Kuku aliazima sindano lakini akachoka kushona baada ya muda mfupi. Akaacha sindano kabatini na akaenda jikoni kuandaa chakula kwa ajili ya watoto wake.
Aber die anderen Vögel hatten Adler davonfliegen sehen. Sie baten Henne, ihnen die Nadel zu leihen, um sich selbst auch Flügel zu nähen. Schon bald flogen am ganzen Himmel Vögel.
Lakini ndege wengine walimwona Tai akipaa. Wakamwomba Kuku awaazime sindano ili nao wajishonee mabawa pia. Muda si mrefu ndege wakawa wamepaa na kuzagaa anga zima.
Als der letzte Vogel die geliehene Nadel zurückbrachte, war Henne nicht da. Also nahmen ihre Kinder die Nadel und spielten damit. Als sie keine Lust mehr am Spielen hatten, ließen sie die Nadel im Sand liegen.
Ndege wa mwisho aliporudisha sindano aliyoazima, Kuku hakuwepo. Kwa hiyo watoto wake wakachukua sindano na wakaanza kuichezea. Walipochoka na mchezo wao, wakaiacha sindano kwenye mchanga.
Später am Nachmittag kam Adler zurück. Sie fragte nach der Nadel, um einige Federn, die sich beim Flug gelockert hatten, zu reparieren. Henne sah auf dem Schrank nach. Sie sah in der Küche nach. Sie sah im Garten nach. Aber die Nadel war nirgends zu finden.
Baadaye jioni Tai akarudi. Akaomba sindano ili aweze kushona baadhi ya manyoya yaliyokuwa yameanza kulegea alipokuwa safarini. Akaangalia kwenye kabati. Akaangalia jikoni. Akaangalia uani. Ila sindano haikupatikana.
„Gib mir bloß einen Tag“, bat Henne Adler. „Dann kannst du deinen Flügel reparieren und davonfliegen, um Essen zu holen.“ „Nur ein Tag“, sagte Adler, „Wenn du die Nadel bis dann nicht findest, musst du mir eins deiner Küken zur Wiedergutmachung geben.“
“Nipatie siku moja,” Kuku alimwomba Tai. “Halafu utaweza kushona bawa lako na kuruka tena kwenda kutafuta chakula.” “Siku moja tu,” alisema Tai. “Kama hutaipata sindano, itabidi unipe kimoja cha vifaranga vyako kama malipo.”
Als Adler am nächsten Tag vorbeikam, fand sie Henne im Sand scharren, aber ohne Nadel. Daher ging Adler in den Sturzflug und schnappte sich eins der Küken. Sie trug es davon. Seitdem, immer wenn Adler auftaucht, sieht sie Henne im Sand auf der Suche nach der Nadel scharren.
Tai aliporudi siku iliyofuata, alimkuta Kuku akichakura mchangani, ila hakukuwa na sindano. Kwa hiyo Tai alishuka kwa kasi na kukwapua kifaranga kimoja. Akaondoka nacho. Tangu hapo, kila Tai anapojitokeza humkuta Kuku akichakura kwenye mchanga akitafuta sindano.
Wenn Adlers Flügel Schatten auf den Boden werfen, warnt Henne ihre Küken: „Meidet das freie und trockene Land.“ Und sie antworten: „Wir sind keine Narren. Wir werden laufen.“
Kila kivuli cha mabawa ya Tai kinapoonekana ardhini, Kuku huwatahadharisha vifaranga vyake. “Tokeni kwenye eneo la wazi.” Na wanajibu: “Sisi si wajinga. Tutakimbia.”