Download PDF
Back to stories list

Uamuzi Decision La décision

Written by Ursula Nafula

Illustrated by Vusi Malindi

Translated by Ursula Nafula

Read by Lauwo George

Language Kiswahili

Level Level 2

Narrate full story

Autoplay story


Kijiji changu kilikuwa na matatizo mengi. Tulipanga foleni ndefu tukisubiri kuchota maji kutoka mfereji mmoja.

My village had many problems. We made a long line to fetch water from one tap.

Mon village avait beaucoup de problèmes. Nous faisions la queue pour aller chercher de l’eau d’un seul robinet.


Tulisubiri kupokea msaada wa chakula.

We waited for food donated by others.

Nous attendions la nourriture donnée par les autres.


Tulifunga nyumba zetu mapema kwasababu ya wizi.

We locked our houses early because of thieves.

Nous barrions nos maisons tôt à cause des voleurs.


Watoto wengi waliacha shule.

Many children dropped out of school.

Plusieurs enfants avaient abandonné l’école.


Wasichana wadogo walifanya kazi za nyumbani kwenye vijiji vingine.

Young girls worked as maids in other villages.

Les jeunes filles travaillaient comme domestiques dans d’autres villages.


Wavulana wadogo waliranda randa kijijini na wengine walifanya kazi kwenye mashamba ya watu.

Young boys roamed around the village while others worked on people’s farms.

Les jeunes garçons se promenaient autour du village pendant que d’autres travaillaient sur des fermes.


Upepo ulipovuma, ulipeperusha karatasi chafu na kuzifikisha mitini na uani.

When the wind blew, waste paper hung on trees and fences.

Quand le vent soufflait, des déchets de papier pendaient des arbres et des clôtures.


Watu walikatwa na vipande vya chupa vilivyotupwa ovyo ovyo.

People were cut by broken glass that was thrown carelessly.

Les gens se faisaient couper par de la vitre brisée lancée sans faire attention.


Halafu siku moja, mfereji wa maji ulikauka na mitungi yetu ikawa mitupu.

Then one day, the tap dried up and our containers were empty.

Puis un jour, le robinet se tarit et nos conteneurs étaient vides.


Baba yangu alitembea nyumba hadi nyumba akiwaomba watu kuhudhuria mkutano wa kijiji.

My father walked from house to house asking people to attend a village meeting.

Mon père marcha de maison en maison et demanda aux gens de participer à une réunion du village.


Watu walikusanyika chini ya mti mkubwa na kusikiliza.

People gathered under a big tree and listened.

Les gens se rassemblèrent sous un grand arbre et écoutèrent.


Baba yangu alisimama na kusema, “Tunahitaji kusaidiana kutatua matatizo yetu.”

My father stood up and said, “We need to work together to solve our problems.”

Mon père se leva et dit, « Nous devons travailler ensemble pour résoudre nos problèmes. »


Juma, mtoto wa miaka minane aliyekuwa amekaa kwenye tawi la mti, alisema kwa sauti, “Naweza kusaidia na usafi.”

Eight-year-old Juma, sitting on a tree trunk shouted, “I can help with cleaning up.”

Juma, âgée de huit ans et assise sur un tronc d’arbre, cria, « Je peux aider à nettoyer. »


Mwanamke mmoja alisema, “Sisi wanawake tunaweza kuungana na kulima.”

One woman said, “The women can join me to grow food.”

Une femme dit, « Les femmes peuvent me joindre pour faire pousser de la nourriture. »


Mwanamume mwingine alisimama na kusema, “Wanaume watachimba kisima cha maji.”

Another man stood up and said, “The men will dig a well.”

Un autre homme se leva et dit, « Les hommes creuseront un puits. »


Sote tulisema kwa sauti moja, “Lazima tubadilishe maisha yetu.” Tangu siku hiyo, tulifanya kazi pamoja kutatua shida zetu.

We all shouted with one voice, “We must change our lives.” From that day we worked together to solve our problems.

Nous criions tous d’une seule voix, « Nous devons changer nos vies. » Depuis ce jour, nous avons travaillé ensemble pour résoudre nos problèmes.


Written by: Ursula Nafula
Illustrated by: Vusi Malindi
Translated by: Ursula Nafula
Read by: Lauwo George
Language: Kiswahili
Level 2
Source: Decision from African Storybook
Creative Commons License
This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
Options
Back to stories list Download PDF