Back to stories list
निर्णय
Uamuzi
Decision
Ursula Nafula
Vusi Malindi
Nandani
The audio for this story is currently not available.
मेरे गाँव में बहुत सारी समस्याएँ थीं। हमें नल से पानी लेने के लिए बहुत लंबी लाइन लगानी पड़ती थी।
Kijiji changu kilikuwa na matatizo mengi. Tulipanga foleni ndefu tukisubiri kuchota maji kutoka mfereji mmoja.
My village had many problems.
We made a long line to fetch water from one tap.
हमें दूसरों द्वारा दिए गए भोजन का इंतज़ार करना पड़ता था।
Tulisubiri kupokea msaada wa chakula.
We waited for food donated by others.
चोरों के कारण हमें अपने घर जल्दी बंद करने पड़ते थे।
Tulifunga nyumba zetu mapema kwasababu ya wizi.
We locked our houses early because of thieves.
बहुत से बच्चों ने बीच में ही स्कूल छोड़ दिया।
Watoto wengi waliacha shule.
Many children dropped out of school.
नौजवान लड़कियाँ दूसरे गाँव में नौकरानी का काम करती थीं।
Wasichana wadogo walifanya kazi za nyumbani kwenye vijiji vingine.
Young girls worked as maids in other villages.
नौजवान लड़के गाँव में घूमते रहते थे जबकि बाकी दूसरों के खेतों में काम करते थे।
Wavulana wadogo waliranda randa kijijini na wengine walifanya kazi kwenye mashamba ya watu.
Young boys roamed around the village while others worked on people’s farms.
जब हवा चलती तो बेकार पड़े कागज़, पेड़ों और बाड़ों से लटक जाते थे।
Upepo ulipovuma, ulipeperusha karatasi chafu na kuzifikisha mitini na uani.
When the wind blew, waste paper hung on trees and fences.
लापरवाही से फेंके गए काँच के टुकड़ों से लोग घायल हो जाते थे।
Watu walikatwa na vipande vya chupa vilivyotupwa ovyo ovyo.
People were cut by broken glass that was thrown carelessly.
फिर एक दिन, नल सूख गये और हमारे बर्तन खाली रह गए।
Halafu siku moja, mfereji wa maji ulikauka na mitungi yetu ikawa mitupu.
Then one day, the tap dried up and our containers were empty.
मेरे पिता ने घर-घर जाकर लोगों से विनती की कि वे गाँव की बैठक में आएँ।
Baba yangu alitembea nyumba hadi nyumba akiwaomba watu kuhudhuria mkutano wa kijiji.
My father walked from house to house asking people to attend a village meeting.
एक बड़े पेड़ के नीचे लोग इकट्ठे हुए और उन्होंने सुना।
Watu walikusanyika chini ya mti mkubwa na kusikiliza.
People gathered under a big tree and listened.
मेरे पिता ने खड़े होकर कहा “हमारी समस्याओं को सुलझाने के लिए हमें साथ मिलकर काम करना होगा”।
Baba yangu alisimama na kusema, “Tunahitaji kusaidiana kutatua matatizo yetu.”
My father stood up and said, “We need to work together to solve our problems.”
पेड़ की डाली पर बैठा आठ वर्षीय जुमा चिल्लाया “मैं सफाई में मदद कर सकता हूँ”।
Juma, mtoto wa miaka minane aliyekuwa amekaa kwenye tawi la mti, alisema kwa sauti, “Naweza kusaidia na usafi.”
Eight-year-old Juma, sitting on a tree trunk shouted, “I can help with cleaning up.”
एक महिला ने कहा “महिलाएँ मेरे साथ मिलकर फ़सल उगा सकती हैं”।
Mwanamke mmoja alisema, “Sisi wanawake tunaweza kuungana na kulima.”
One woman said, “The women can join me to grow food.”
एक और आदमी खड़ा हुआ और बोला “आदमी कुआँ खोदेंगे”।
Mwanamume mwingine alisimama na kusema, “Wanaume watachimba kisima cha maji.”
Another man stood up and said, “The men will dig a well.”
हमने साथ मिलकर एक स्वर में ज़ोर से कहा “हम अपनी ज़िंदगी ज़रूर बदलेंगे”। उस दिन से हम अपनी समस्याओं को हल करने के लिए साथ काम करते हैं।
Sote tulisema kwa sauti moja, “Lazima tubadilishe maisha yetu.” Tangu siku hiyo, tulifanya kazi pamoja kutatua shida zetu.
We all shouted with one voice, “We must change our lives.”
From that day we worked together to solve our problems.
Written by: Ursula Nafula
Illustrated by: Vusi Malindi
Translated by: Nandani