有一天,兔子在河边散步。
Siku moja, Sungura alikuwa akitembea pembeni ya mto.
河马也在那儿,一边闲逛,一边找些美味的野草来吃。
Kiboko alikuwepo pia, akitembea huku akila majani mazuri ya kijani.
河马没有看见兔子,她不小心踩到了兔子的脚。兔子尖叫了一声,朝着河马大喊:“该死的河马!没看到你踩到我的脚了吗?”
Kiboko hakumwona Sungura na kwa bahati mbaya akaukanyaga mguu wa Sungura. Sungura akaanza kumpigia Kiboko kelele. “We Kiboko huoni kama umeukanyaga mguu wangu?”
河马赶紧给兔子道歉:“真不好意思,我的朋友!我没看见你!请原谅我!”兔子哪里会听河马的解释,他气极了,朝着河马大吼:“你肯定是故意的!总有一天你会受到惩罚!”
Kiboko akamwomba Sungura msamaha, “Samahani, sikukuona, tafadhali nisamehe!” Lakini Sungura hakukubali na akaendelea kumbwatukia Kiboko, “Umefanya makusudi! Kuna siku utakiona, na nitakulipizia!”
兔子找到了火,他对火说:“趁河马从水里出来吃草的时候,朝她放一把火。她竟敢踩我的脚。”火回答说:“没问题,我的朋友!我这就按你说的做。”
Sungura alienda kumtafuta moto na akamwambia, “Nenda, ukamchome Kiboko akitoka majini kuja kula majani. Alinikanyaga!” Moto ukajibu, “Hakuna tatizo, rafiki yangu Sungura, nitafanya ulichoniomba kufanya.”
过了一会儿,河马正在离河岸很远的地方吃草。呼的一声,火突然烧起来了,烧到了河马的身上。
Baadaye, Kiboko alikuwa akila majani mbali na mto, aliposhtuka moto umelipuka. Miale ya moto ikaanza kuzichoma nywele za Kiboko.
河马尖叫着,赶紧跑向河边,但是她的毛发已经全部烧毁了。河马伤心地说:“我的毛都被火烧掉了!你烧了我的毛!它们全都不见了!我美丽的毛!”
Kiboko akaanza kulia na kukimbilia kwenye maji. Nywele zake zote zilikuwa zimeungua na moto. Kiboko aliendelea kulia, “Nywele zangu zimeungua na moto! Nywele zangu zote zimeisha! Nywele zangu nzuri!”
兔子终于报了仇,他高兴坏了;直到现在,河马也不敢离河岸太远,因为她害怕又要被火烧。
Sungura alikuwa na furaha kwa kuwa nywele za Kiboko ziliungua. Hadi leo kwa kuogopa moto, Kiboko hawezi kwenda mbali na maji.