Download PDF
Back to stories list

诺孜贝儿和三根头发 Nozibele na nywele tatu

Written by Tessa Welch

Illustrated by Wiehan de Jager

Translated by Vicky Liu

Read by Zhuo Sun

Language Chinese (Mandarin)

Level Level 3

Narrate full story

Reading speed

Autoplay story


很久很久以前,有三个女孩,她们一起外出找柴火。

Hapo zamani za kale, wasichana watatu walienda kukusanya kuni.


天很热,她们跳下河游了个泳。她们一边游泳,一边嬉戏,溅出很多水花。

Ilikuwa ni siku yenye jua kali na wakaamua kwenda mtoni kuogelea. Wakaogelea huku wakicheza na kurushiana maji.


突然,她们意识到天已经很晚了,匆匆忙忙赶回村子。

Ghafla waligundua kuwa muda umekwenda. Wakaharakisha kurudi nyumbani.


当她们快到家的时候,诺孜贝儿摸了摸她的脖子:她把项链落在了外面。于是她请求她的朋友们:“和我一起回去找找吧!”但她的朋友们都说太晚了。

Walipokuwa wanakaribia kufika nyumbani, Nozibele akajishika shingoni. Alikuwa amesahau shanga zake! “Tafadhali turudini!” aliwasihi rafiki zake. Lakini rafiki zake wakasema tumechelewa.


诺孜贝儿一个人回到河边,一找到了项链,就赶忙回家,但天太黑了,她迷路了。

Kwa hiyo Nozibele akarudi mwenyewe mtoni. Akapata shanga zake na akakimbia kurudi nyumbani. Lakini akapotea gizani.


她远远地看见有个小木屋,木屋里有一丝光亮。她跑到木屋门口,敲了敲门。

Kwa mbali akaona mwanga unatoka kwenye nyumba. Akakimbilia kwenye nyumba na kugonga mlango.


诺孜贝儿吃了一惊,开门的是一只会说话的狗:“你来干嘛?”诺孜贝儿说:“我迷路了,我要找个地方睡觉。”狗回答说:“进来吧,不然我就咬你!”然后诺孜贝儿就进了屋。

Akastaajabu kumwona mbwa akifungua mlango na akasema, “Unataka nini?” “Nimepotea na ninatafuta sehemu ya kulala,” akasema Nozibele. “Ingia ndani, la sivyo nitakung’ata!” mbwa akamwambia. Nozibele akaingia ndani.


狗说:“给我做饭!”诺孜贝儿回答说:“但我从来没有给狗做过饭。”狗说:“快做饭,不然我就咬你。”诺孜贝儿没办法,只能给狗做了一些吃的。

Mbwa akamwambia, “Nipikie!” “Sijawahi kumpikia mbwa,” akajibu. “Pika, la sivyo nitakung’ata!” mbwa akasema. Nozibele akampikia mbwa chakula.


狗说:“给我铺床!”诺孜贝儿回答说:“但我从来没有给狗铺过床。”狗说:“快铺床,不然我就咬你。”诺孜贝儿没办法,只能给狗铺了床。

Mbwa akamwambia, “Nitandikie kitanda!” Nozibele akajibu, “Sijawahi kumtandikia mbwa kitanda.” “Tandika kitanda, la sivyo nitakung’ata!” mbwa akasema. Nozibele akatandika kitanda.


诺孜贝儿每天都要给狗做饭,打扫屋子,洗衣服。有一天,狗说:“诺孜贝儿,我今天要出门见朋友。在我回来之前,你要打扫好屋子,做好饭,洗好衣服。”

Akawa kila siku anampikia, anamfulia na kumfagilia mbwa. Siku moja mbwa akasema, “Nozibele, leo naenda kuwatembelea rafiki zangu. Fagia nyumba, pika chakula na osha vitu vyangu kabla sijarudi.”


狗一走,诺孜贝儿就从头上拔了三根头发下来。她把一根头发放在床下,一根放在门背后,还有一根放在篱笆上。然后诺孜贝儿用尽全力跑回了家。

Mara baada tu ya mbwa kuondoka, Nozibele akanyofoa nywele tatu kutoka kwenye kichwa chake. Akaweka unywele mmoja chini ya kitanda, mmoja nyuma ya mlango, na mwingine akauweka kwenye uzio wa nyumba. Halafu, akakimbia kuelekea nyumbani kwa nguvu zote.


当狗回到家的时候,它开始找诺孜贝儿:“诺孜贝儿,你在哪里?”第一根头发说:“我在这儿,在床底下。”第二根头发说:“我在这儿,在门背后。”第三根头发说:“我在这儿,在篱笆上。”

Mbwa aliporudi akaanza kumtafuta Nozibele. “Nozibele, uko wapi?” akapiga kelele. “Niko hapa, chini ya kitanda,” unywele wa kwanza ukajibu. “Nipo hapa nyuma ya mlango,” unywele wa pili ukajibu. “Niko hapa kwenye uzio,” unywele wa tatu ukajibu.


狗明白了诺孜贝儿耍的花招。它一路跑到诺孜贝儿的村庄,但是诺孜贝儿的兄弟们正拿着棍子等着它呢!狗见状不妙,赶紧跑开了,从此再也没人见过它。

Mbwa akagundua kuwa Nozibele amemkimbia. Kwa hiyo akakimbia kuelekea kijijini. Kaka zake Nozibele walikuwa wakimsubiri na fimbo. Mbwa alipowaona akageuka na kukimbia, na hajawahi kuonekana tena.


Written by: Tessa Welch
Illustrated by: Wiehan de Jager
Translated by: Vicky Liu
Read by: Zhuo Sun
Language: Chinese (Mandarin)
Level: Level 3
Source: Nozibele and the three hairs from African Storybook
Creative Commons License
This work is licensed under a Creative Commons Attribution 3.0 International License.
Options
Back to stories list Download PDF