山羊、野狗、和水牛是很要好的朋友。有一天,他们一起坐出租车。
Mbuzi, Mbwa na Ng’ombe walikuwa marafiki wa karibu sana. Siku moja walisafiri kwa teksi.
当他们到了目的地的时候,司机叫他们交车费。水牛把她自己的那份交了。
Walipofika mwisho wa safari yao, dereva aliwaomba walipe nauli zao. Ng’ombe alilipa nauli yake.
野狗没有带零钱,所以他就多给了一点儿。
Mbwa alilipa zaidi kidogo kwa sababu hakuwa na pesa taslimu.
司机正要找钱给野狗,没想到山羊没有给钱就跑掉了。
Dereva alipokaribia kumpa Mbwa chenji yake, Mbuzi alitoroka bila kulipa chochote.
司机很生气,结果他没有给野狗找钱就开走了。
Dereva alikasirika sana. Aliondoka bila kumrudishia Mbwa chenji yake.
所以,现在你可以看到野狗看到车子就拼命追上去,因为他想叫司机给他找钱。
Hiyo ndiyo sababu hadi leo Mbwa hukimbiza magari ili achungulie ndani kuona kama atampata dereva mwenye chenji yake.
山羊呢,一听到有车来就吓得赶快逃走,因为她怕没交车费被人抓起来。
Mbuzi hukimbia anaposikia mlio wa gari. Anaogopa atakamatwa kwa kutolipa nauli.
可是水牛听到车来一点儿都不急。她不慌不忙地过马路,因为她知道她已经把她自己那份交了。
Na Ng’ombe hababaiki gari likiwa linakuja. Ng’ombe huvuka barabara bila wasiwasi kwa sababu anajua alilipa nauli yake yote.