Kuku na Jongoo walikuwa marafiki. Ila walikuwa wanashindana kila mara. Siku moja wakaamua kucheza mpira wa miguu ili waweze kubaini nani alikuwa mchezaji bora zaidi.
Wakaenda uwanjani na wakaanza kucheza. Kuku alikuwa na kasi ila Jongoo alikuwa na kasi zaidi. Kuku alipiga mpira mbali, ila Jongoo alipiga mbali zaidi. Kuku akaanza kupandwa na hasira.
Kuku alipokuwa anarudi nyumbani alikutana na Mama yake Jongoo. Mama Jongoo akamuuliza, “Umemwona mwanangu?” Kuku hakujibu kitu. Mama Jongoo akapatwa na wasiwasi.
Mama Jongoo akasikia sauti kwa mbali. “Nisaidie mama!” ile sauti ililia. Mama Jongoo akaangalia huku na kule na kusikiliza kwa makini. Sauti ilitokea tumboni mwa kuku.
Mama Jongoo alipiga kelele, “Tumia nguvu yako ya kipekee mwanangu!” Majongoo wanaweza kutoa harufu mbaya na ladha ya ajabu. Kuku akaanza kujisikia mgonjwa.