Wakaanza kubishana. “Tulisema tutawaweka mama na mtoto salama, na hivyo ndivyo tutakavyofanya,” baadhi wakasema. “Lakini watatuletea mkosi!” wengine wakadai.
Kwa hiyo mwanamke yule alijikuta yuko peke yake kwa mara nyingine tena. Akajiuliza atafanya nini na mtoto huyo wa ajabu. Akajiuliza atafanya nini na yeye mwenyewe.
Endapo mtoto huyo angebaki kuwa vilevile, na umbo dogo, labda kila kitu kingekuwa tofauti. Lakini mtoto Punda aliendelea kukua na kukua mpaka hakuweza kutoshea tena mgongoni mwa mama yake. Pamoja na kujaribu kwa bidii, hakuweza kuwa na tabia za kibinadamu. Mara nyingi mama yake alichoka na kuvunjika moyo. Wakati mwingine alimlazimisha kufanya kazi walizostahili wanyama.
Kuchanganyikiwa na hasira vilianza kujengeka ndani mwa Punda. Alishindwa kufanya hivi wala vile. Alishindwa kuwa hivi wala vile. Alipatwa na hasira sana kiasi kwamba, siku moja, alimpiga teke mama yake mpaka akaanguka chini.
Epunda neryo muyayiswekera. Yamathibitha hali omwirungu.
Punda alijawa na aibu. Akaanza kukimbilia mbali kwa haraka kadiri awezavyo.
Wakati aliposimama, ilikuwa ni usiku, na alikuwa amepotea. “Hii hoo?” alinong’ona gizani. “Hii hoo?” giza likatoa mwangwi. Alikuwa mwenyewe. Alijikunyata katika umbo dogo, akalala fofofo usingizi wa mang’amung’amu.
Punda alienda kuishi na mzee yule, na mzee alimfundisha mbinu nyingi za kuishi. Punda alisikiliza na kujifunza, na mzee vivyo hivyo pia. Walisaidiana na kucheka pamoja.