Kituo kidogo cha mabasi kijijini mwetu kilijaa shughuli za watu na mabasi. mabasi mengi yalikuwa yamejaa mizigo. Chini, palikuwa na mizigo zaidi ya kupakia. Makondakta walikuwa wanataja majina ya sehemu mabasi yalikokuwa yanaelekea.
「街!街!西行き!」僕は客引きが叫んでいるのを聞いた。あれは僕の乗らないといけないバスだった。
“Mjini! Mjini! Magharibi!” Nilisikia kondakta akiita kwa sauti. Lile ndilo basi nililohitaji kupanda.
Basi la kwenda mjini lilikaribia kujaa, lakini watu wengine walikuwa wanasukumana kupanda. Baadhi yao walipakia mizigo chini ya basi. Wengine waliiweka katika sehemu ya juu.
Nilijipenyeza ndani na kukaa karibu na dirisha. Mtu aliyeketi karibu nami alishika mfuko wa plastiki wa kijani kibichi. Alivaa viatu vilivyochakaa, koti kuukuu na alionekana kuwa na wasiwasi.
僕は外を見て、僕の育った村を離れることを再確認した。僕は大きな街に行くのだ。
Niliangalia nje na kutambua kwamba nilikuwa naondoka kijijini kwangu, mahali ambapo nililelewa. Nilikuwa naenda katika mji mkubwa.
Upakiaji mizigo ulikamilika na abiria wakawa wameketi. Wachuuzi walizidi kusukumana kutaka kuingia ndani ya basi ili wauze bidhaa zao. Kila mmoja alitaja kwa sauti majina ya bidhaa alizokuwa anauza. Maneno yao yalinifurahisha.
Wachuuzi walisukumana huku wakitafuta njia ya kushuka. Wengine waliwarudishia wasafiri chenji zao. Wengine walifanya juhudi za mwisho kuuza bidhaa zao.
Lakini mawazo yangu yalirejea nyumbani. Je, mamangu atakuwa salama? Je, sungura wangu wataleta hela zozote? Je, ndugu yangu atakumbuka kunyunyizia maji miche ya miti yangu?
Basi la kurudi lilikuwa linajaa upesi. Muda mfupi baadaye, lingeanza safari ya kwenda mashariki. Jambo la maana kwangu wakati huo lilikuwa kuanza kutafuta nyumba ya mjomba wangu.