Download PDF
Back to stories list

おばあさんとの休日 Likizo kwa bibi

Written by Violet Otieno

Illustrated by Catherine Groenewald

Translated by Maaya UCHIMURA

Read by Yumi Okano

Language Japanese

Level Level 4

Narrate full story

Reading speed

Autoplay story


オドンゴとアピヨは、お父さんと都会に住んでいました。彼らは休日を楽しみにしていました。ただ学校を休めるからではなく、おばあさんに会いに行けるからです。おばあさんは大きな湖の近くにある漁村に住んでいました。

Odongo na Apiyo waliishi mjini na baba yao. Walisubiri likizo kwa hamu. Siyo tu kwa shule kufungwa, bali ni kwa sababu walienda kumtembelea bibi yao. Aliishi katika kijiji cha uvuvi karibu na ziwa kubwa.


オドンゴとアピヨは、またおばあさんのところに遊びに行けることができて、わくわくしていました。前日の夜、鞄に荷物を詰めて、村までの長旅の準備をしました。眠れず、一晩中休日の話をしました。

Odongo na Apiyo walichangamka kwani ulikuwa wakati wa kumtembelea bibi kwa mara nyingine. Usiku huo, walipanga mizigo yao na kujiandaa kwa safari ndefu ya kwenda kijijini. Hawakuweza kulala ila waliongea usiku kucha juu ya likizo yao.


次の日の朝早く、お父さんの車で村に向けて出発しました。山々や野生動物、茶畑を車で通り過ぎました。車を数え、歌を歌いました。

Mapema asubuhi iliyofuata, waliondoka katika gari la baba yao kuelekea kijijini. Walipita milima, wanyama pori na mashamba ya majani ya chai. Walihesabu magari na kuimba nyimbo.


しばらくして子どもたちは疲れて眠ってしまいました。

Baada ya muda, watoto walichoka na kusinzia.


村に着くと、お父さんはオドンゴとアピヨを起こしました。彼らのおばあさん、ニャル・カニャダが木陰のマットの上で休んでいるのを見つけました。ニャル・カニャダとはルオ語で「カニャダの民の娘」という意味です。彼女は強く美しい女性です。

Baba aliwaamsha Odongo na Apiyo walipofika kijijini. Walimkuta bibi yao, Nyar-Kanyada, akipumzika kwenye mkeka chini ya mti. Kwa Dholuo, Nyar-Kanyada maana yake ni ‘binti wa watu wa Kanyada’. Alikuwa ni mwanamke mrembo na imara.


ニャル・カニャダは彼らを家に迎え入れ、歓喜のあまり歌いながら部屋中を踊りまわりました。孫たちははしゃいで、都会から持ってきたプレゼントをおばあさんに渡しました。「まず僕のプレゼントを開けて」とオドンゴが言いました。「ダメ、私のプレゼントが先!」とアピヨが言いました。

Nyar-Kanyada aliwakaribisha ndani kwa kucheza na kuimba kwa furaha. Wajukuu wake walikuwa na shauku ya kumpa zawadi walizomletea kutoka mjini. “Fungua yangu kwanza,” Odongo alisema. “Hapana, yangu kwanza!” Apiyo akasema.


プレゼントを開けてから、ニャル・カニャダは昔から伝わるやり方で孫たちに感謝しました。

Baada ya kufungua zawadi, Nyar-Kanyada aliwabariki wajukuu wake kitamaduni.


それからオドンゴとアピヨは出かけました。蝶々や鳥を追いかけました。

Kisha Odongo na Apiyo wakaenda nje. Waliwakimbiza vipepeo na ndege.


木登りをし、湖で水遊びをしました。

Walipanda kwenye miti na kurushiana maji ziwani.


暗くなって、晩御飯を食べに家に帰りました。食べ終える前に彼らは眠りに落ちていました!

Giza Iilipoingia, walirudi nyumbani kwa ajili ya chakula cha jioni. Kabla hata ya kumaliza kula, walikuwa wanasinzia!


次の日、お父さんは子どもたちをニャル・カニャダのもとに残して都会へ車で戻りました。

Siku iliyofuata, baba yao alirudi mjini na kuwaacha na Nyar-Kanyada.


オドンゴとアピヨは家事を手伝いました。水を汲み、薪を集めました。鶏から卵を集め、庭で野菜を採りました。

Odongo na Apiyo walimsaidia bibi yao na kazi za nyumbani. Walichota maji na kuokota kuni. Walikusanya mayai ya kuku na kuchuma mboga za majani kutoka kwenye bustani.


ニャル・カニャダは、シチューと一緒に食べる柔らかいウガリの作り方を孫に教えました。焼き魚と一緒に食べるココナッツ・ライスの作り方も教えました。

Nyar-Kanyada aliwafundisha wajukuu wake jinsi ya kupika ugali mwepesi wa kula na mchuzi. Aliwaonesha namna ya kupika wali wa nazi wa kuliwa na samaki wa kukaanga.


ある朝、オドンゴはおばあさんの牛を連れて、草を食べさせに行きました。しかし牛たちは近所の人の畑に走っていきました。農家の人はオドンゴに腹を立てました。牛たちが作物を食べないようにしろと脅しました。その日から、オドンゴは牛たちがまた問題を起こさないように気をつけました。

Asubuhi moja, Odongo aliwapeleka ng’ombe wa bibi yake malishoni. Wakakimbilia ndani ya shamba la jirani. Mwenye shamba alikasirishwa sana na Odongo. Akatishia kuwazuia ng’ombe kula mimea yake. Tangu siku hiyo, Odongo alihakikisha kwamba ng’ombe hawaingii matatani tena.


別の日に、子どもたちはニャル・カニャダと一緒に市場に行きました。彼女は野菜や砂糖、石けんを売る屋台をやっていました。アピヨはお客さんに商品の値段を教えるのが好きでした。オドンゴはお客さんが買った商品を詰める係でした。

Siku nyingine watoto walikwenda sokoni pamoja na Nyar-Kanyada. Nyar-Kanyada alikuwa na kibanda cha kuuza mboga, sukari na sabuni. Apiyo alipenda kuwatajia wateja bei za bidhaa. Odongo aliwafungia wateja bidhaa walizonunua.


一日の終わりに、一緒にチャイを飲みました。彼らはおばあさんが稼いだお金を数えるのを手伝いました。

Mwisho wa siku walikunywa chai pamoja. Walimsaidia bibi yao kuhesabu pesa alizozipata.


しかし、あまりにも早くに休日が終わってしまい、子どもたちは都会に戻らなければならなくなりました。ニャル・カニャダはオドンゴには帽子を、アピヨにはセーターをあげました。旅のために食べ物を詰めました。

Likizo ilikaribia kuisha na watoto walitakiwa kurudi mjini. Nyar-Kanyada alimpa Odongo kofia na Apiyo sweta. Aliwafungia chakula cha kula safarini.


お父さんが迎えに来たとき、彼らは帰りたくありませんでした。子どもたちはニャル・カニャダに一緒に都会に来るようお願いしました。彼女は笑って「私は都会には歳を取りすぎているわ。あなたたちがまた村に来るのを待っているよ」と言いました。

Baba yao alipokuja kuwachukua, hawakutaka kuondoka. Walimuomba Nyar-Kanyada aende nao mjini. Alitabasamu na kusema, “Nimezeeka, siyawezi ya mjini. Nitasubiri mje kijijini kwangu tena.”


オドンゴとアピヨは二人とも、おばあさんを強く抱きしめ、さよならを言いました。

Odongo na Apiyo walimkumbatia kwa pamoja na kumuaga.


オドンゴとアピヨは学校に戻って、友だちに村での生活について話しました。都会の生活がいいと思う友だちもいました。村の方がいいと思う子もいました。でも何より、オドンゴとアピヨには素敵なおばあさんがいるということでみんな意見が一致しました!

Odongo na Apiyo waliporudi shuleni, waliwasimulia marafiki zao kuhusu maisha ya kijijini. Baadhi ya watoto waliamini kuwa maisha ya mjini ni mazuri. Wengine waliamini kijijini ni bora zaidi. Lakini zaidi ya yote, kila mmoja alikubali kwamba Odongo na Apiyo walikuwa na bibi wa kipekee.


Written by: Violet Otieno
Illustrated by: Catherine Groenewald
Translated by: Maaya UCHIMURA
Read by: Yumi Okano
Language: Japanese
Level: Level 4
Source: Holidays with grandmother from African Storybook
Creative Commons License
This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
Options
Back to stories list Download PDF