Download PDF
Back to stories list

Alichokisema dada yake Vusi What Vusi's sister said @alichokisema @dada jake @vusi

Written by Nina Orange

Illustrated by Wiehan de Jager

Translated by Matteo E. Mwita

Read by Lauwo George

Language Kiswahili

Level Level 4

Narrate full story

Autoplay story


Siku moja asubuhi bibi yake Vusi alimwita na kumwambia, “Tafadhali peleka yai hili kwa wazazi wako. Wanataka kutengeneza keki kubwa kwa ajili ya harusi ya dada yako.”

Early one morning Vusi’s granny called him, “Vusi, please take this egg to your parents. They want to make a large cake for your sister’s wedding.”

siku moʄa asuɓuhi ɓiɓi jake @vusi alimwita na kumwaᵐɓia tafaɗhali peleka jai hili kwa wazazi wako wanataka kuteᵑgeneza keki kuɓwa kwa aʄili ja haɾusi ja @dada jako


Alipokuwa njiani kuelekea kwa wazazi wake, Vusi akakutana na vijana wawili wanaokota matunda. Kijana mmoja akanyakua yai kutoka kwa Vusi na akalirusha kwenye mti. Yai likavunjika.

On his way to his parents, Vusi met two boys picking fruit. One boy grabbed the egg from Vusi and shot it at a tree. The egg broke.

alipokuwa ⁿɗʒiani kuelekea kwa wazazi @wake @vusi akakutana na viʄana wawili wanaokota matuⁿɗa kiʄana mmoʄa @akanyakua jai kutoka kwa @vusi na @akalirusha kweɲe mti jai @likavunjika


“Umefanya nini?” Vusi akalia. “Yai lile lilikuwa kwa ajili ya keki. Keki ilikuwa kwa ajili ya harusi ya dada yangu. Dada yangu atasemaje kama hakutakuwa na keki ya harusi?”

“What have you done?” cried Vusi. “That egg was for a cake. The cake was for my sister’s wedding. What will my sister say if there is no wedding cake?”

umefaɲa nini @vusi akalia jai lile lilikuwa kwa aʄili ja keki keki ilikuwa kwa aʄili ja haɾusi ja @dada jaᵑgu @dada jaᵑgu @atasemaje kama hakutakuwa na keki ja haɾusi


Vijana wale waliomba msamaha kwa kumchokoza Vusi. “Hatuna la kufanya kuhusu keki, lakini hii hapa ni fimbo kwa ajili ya dada yako,” mmoja alisema. Vusi akaendelea na safari yake.

The boys were sorry for teasing Vusi. “We can’t help with the cake, but here is a walking stick for your sister,” said one. Vusi continued on his journey.

viʄana @wale walioᵐɓa msamaha kwa kumtʃokoza @vusi hatuna la kufaɲa kuhusu keki lakini hii hapa ni fiᵐɓo kwa aʄili ja @dada jako mmoʄa alisema @vusi akaeⁿɗelea na safaɾi jake


Njiani alikutana na wanaume wawili wakijenga nyumba. “Tunaweza kutumia hiyo fimbo imara?” mmoja akaomba. Lakini fimbo haikuwa imara kwa kujengea, na ikavunjika.

Along the way he met two men building a house. “Can we use that strong stick?” asked one. But the stick was not strong enough for building, and it broke.

ⁿɗʒiani alikutana na wanaume wawili @wakijenga ɲuᵐɓa tunaweza kutumia hijo fiᵐɓo imaɾa mmoʄa akaoᵐɓa lakini fiᵐɓo haikuwa imaɾa kwa kuʄeᵑgea na @ikavunjika


“Mmefanya nini?” Vusi akalia. “Fimbo hii ilikuwa zawadi kwa ajili ya dada yangu. Waangua matunda walinipa fimbo hiyo kwa sababu walivunja yai la keki. Keki ilikuwa ni kwa ajili ya harusi ya dada yangu. Sasa hakuna yai, hakuna keki, na hakuna zawadi. Dada yangu atasemaje?”

“What have you done?” cried Vusi. “That stick was a gift for my sister. The fruit pickers gave me the stick because they broke the egg for the cake. The cake was for my sister’s wedding. Now there is no egg, no cake, and no gift. What will my sister say?”

mmefaɲa nini @vusi akalia fiᵐɓo hii ilikuwa zawaɗi kwa aʄili ja @dada jaᵑgu @waangua matuⁿɗa @walinipa fiᵐɓo hijo kwa saɓaɓu @walivunja jai la keki keki ilikuwa ni kwa aʄili ja haɾusi ja @dada jaᵑgu sasa hakuna jai hakuna keki na hakuna zawaɗi @dada jaᵑgu @atasemaje


Wajenzi waliomba msamaha kwa kuvunja fimbo. “Hatuna la kufanya kuhusu keki, lakini tutakupa makuti umpelekee dada yako,” mmoja alisema. Na Vusi akaendelea na safari yake.

The builders were sorry for breaking the stick. “We can’t help with the cake, but here is some thatch for your sister,” said one. And so Vusi continued on his journey.

waʄeⁿzi walioᵐɓa msamaha kwa kuvuⁿɗʒa fiᵐɓo hatuna la kufaɲa kuhusu keki lakini @tutakupa makuti @umpelekee @dada jako mmoʄa alisema na @vusi akaeⁿɗelea na safaɾi jake


Njiani, Vusi akakutana na mkulima akiwa na ng’ombe. “Una makuti mazuri, naweza kupata kidogo?” Ng’ombe akaomba. Lakini makuti yalikuwa matamu ng’ombe akayala yote!

Along the way, Vusi met a farmer and a cow. “What delicious thatch, can I have a nibble?” asked the cow. But the thatch was so tasty that the cow ate it all!

ⁿɗʒiani @vusi akakutana na mkulima akiwa na ŋoᵐɓe una makuti mazuɾi naweza kupata kiɗoɠo ŋoᵐɓe akaoᵐɓa lakini makuti jalikuwa matamu ŋoᵐɓe @akayala jote


“Umefanya nini?” Vusi akalia. “Makuti haya yalikuwa zawadi ya dada yangu. Wajenzi walinipa makuti kwa kuwa walivunja fimbo yangu niliyopewa na waangua matunda. Waangua matunda walinipa fimbo kwa kuwa walivunja yai kwa ajili ya keki ya dada yangu. Keki ilikuwa kwa ajili ya harusi ya dada yangu. Sasa hakuna yai, hakuna keki, na hakuna zawadi. Dada yangu atasemaje?”

“What have you done?” cried Vusi. “That thatch was a gift for my sister. The builders gave me the thatch because they broke the stick from the fruit pickers. The fruit pickers gave me the stick because they broke the egg for my sister’s cake. The cake was for my sister’s wedding. Now there is no egg, no cake, and no gift. What will my sister say?”

umefaɲa nini @vusi akalia makuti haja jalikuwa zawaɗi ja @dada jaᵑgu waʄeⁿzi @walinipa makuti kwa kuwa @walivunja fiᵐɓo jaᵑgu @niliyopewa na @waangua matuⁿɗa @waangua matuⁿɗa @walinipa fiᵐɓo kwa kuwa @walivunja jai kwa aʄili ja keki ja @dada jaᵑgu keki ilikuwa kwa aʄili ja haɾusi ja @dada jaᵑgu sasa hakuna jai hakuna keki na hakuna zawaɗi @dada jaᵑgu @atasemaje


Ng’ombe aliomba msamaha kwa kuwa mlafi. Mkulima alikubali kumpa Vusi ng’ombe aende naye kama zawadi kwa ajili ya dada yake. Vusi akaendelea na safari yake.

The cow was sorry she was greedy. The farmer agreed that the cow could go with Vusi as a gift for his sister. And so Vusi carried on.

ŋoᵐɓe alioᵐɓa msamaha kwa kuwa mlafi mkulima alikuɓali kumpa @vusi ŋoᵐɓe aeⁿɗe naje kama zawaɗi kwa aʄili ja @dada jake @vusi akaeⁿɗelea na safaɾi jake


Lakini wakati wa chakula cha jioni ng’ombe alikimbia kurudi kwa mkulima. Na Vusi akapotea njiani. Akafika kwa kuchelewa sana kwenye harusi ya dada yake. Wageni walikuwa tayari wanakula.

But the cow ran back to the farmer at supper time. And Vusi got lost on his journey. He arrived very late for his sister’s wedding. The guests were already eating.

lakini wakati wa tʃakula tʃa ʄioni ŋoᵐɓe alikiᵐɓia kuɾuɗi kwa mkulima na @vusi akapotea ⁿɗʒiani akafika kwa kutʃelewa sana kweɲe haɾusi ja @dada jake waɠeni walikuwa tajaɾi wanakula


“Nifanye nini?” alilia Vusi. “Ng’ombe aliyekimbia alikuwa ni zawadi, ambayo nilipewa kama mbadala wa makuti niliyopewa na wajenzi. Wajenzi walinipa makuti kwa sababu walivunja fimbo niliyopewa na waangua matunda. Waangua matunda walinipa fimbo kwa sababu walivunja yai la keki. Keki ilikuwa kwa ajili ya harusi. Kwa hiyo hakuna yai, hakuna keki, na hakuna zawadi.”

“What shall I do?” cried Vusi. “The cow that ran away was a gift, in return for the thatch the builders gave me. The builders gave me the thatch because they broke the stick from the fruit pickers. The fruit pickers gave me the stick because they broke the egg for the cake. The cake was for the wedding. Now there is no egg, no cake, and no gift.”

nifaɲe nini alilia @vusi ŋoᵐɓe alijekiᵐɓia alikuwa ni zawaɗi aᵐɓajo nilipewa kama @mbadala wa makuti @niliyopewa na waʄeⁿzi waʄeⁿzi @walinipa makuti kwa saɓaɓu @walivunja fiᵐɓo @niliyopewa na @waangua matuⁿɗa @waangua matuⁿɗa @walinipa fiᵐɓo kwa saɓaɓu @walivunja jai la keki keki ilikuwa kwa aʄili ja haɾusi kwa hijo hakuna jai hakuna keki na hakuna zawaɗi


Dada yake Vusi alifikiria kwa muda, halafu akasema, “Kaka yangu Vusi, usijali zawadi, pia usijali keki! Tupo hapa pamoja, nina furaha. Nenda kavae nguo zako nadhifu na uje tusherehekee siku hii!”

Vusi’s sister thought for a while, then she said, “Vusi my brother, I don’t really care about gifts. I don’t even care about the cake! We are all here together, I am happy. Now put on your smart clothes and let’s celebrate this day!” And so that’s what Vusi did.

@dada jake @vusi @alifikiria kwa muɗa halafu akasema kaka jaᵑgu @vusi usiʄali zawaɗi pia usiʄali keki tupo hapa pamoʄa nina fuɾaha neⁿɗa @kavae ᵑguo zako naɗhifu na uʄe @tusherehekee siku hii


Written by: Nina Orange
Illustrated by: Wiehan de Jager
Translated by: Matteo E. Mwita
Read by: Lauwo George
Language: Kiswahili
Level 4
Source: What Vusi's sister said from African Storybook
Creative Commons License
This work is licensed under a Creative Commons Attribution 3.0 International License.
Options
Back to stories list Download PDF