下载 PDF
返回故事列表

Kuku na Jongoo 鸡和千足虫

作者 Winny Asara

插图 Magriet Brink

译文 Matteo E. Mwita

配音 Lauwo George

语言 斯瓦希里语

级别 3级

将整故事念出来

播放速度

自动念故事


Kuku na Jongoo walikuwa marafiki. Ila walikuwa wanashindana kila mara. Siku moja wakaamua kucheza mpira wa miguu ili waweze kubaini nani alikuwa mchezaji bora zaidi.

鸡和千足虫是好朋友,但是它们又互相竞争。有一天,它们决定进行一场足球比赛,看看谁是最棒的球员。


Wakaenda uwanjani na wakaanza kucheza. Kuku alikuwa na kasi ila Jongoo alikuwa na kasi zaidi. Kuku alipiga mpira mbali, ila Jongoo alipiga mbali zaidi. Kuku akaanza kupandwa na hasira.

它们去了球场,开始比赛。鸡跑得飞快,但是千足虫跑得更快。鸡把球踢得很远,但是千足虫踢得更远。鸡开始有点闷闷不乐。


Wakaamua kupigiana penati. Jongoo akaenda golini. Kuku alifunga goli moja pekee. Ikawa zamu ya kuku kwenda golini.

最后,它们决定来一场点球大战。第一轮中,千足虫当守门员,鸡只拿到了一分。然后,在第二轮中,鸡做守门员。


Jongoo alipiga mpira akafunga. Jongoo akapiga chenga akafunga. Jongoo akapiga kichwa akafunga. Jongoo akafunga magoli matano.

千足虫猛地一踢,球进了。千足虫运球飞快,又进了一球。千足虫跳起来,打了个头球,又得了一分。千足虫一共得了五分。


Kuku akakasirika kwa kuwa amefungwa. Hakuwa mshindani mzuri. Jongoo akaanza kucheka kwa sababu rafiki yake alikuwa analalamika.

鸡输了,它很生气。千足虫哈哈大笑,因为它的朋友输了球,就无理取闹。


Kuku alipatwa na hasira kiasi kwamba akafungua mdomo wake mkubwa na akammeza Jongoo.

鸡生气极了,它张开嘴,一口把千足虫吞了下去。


Kuku alipokuwa anarudi nyumbani alikutana na Mama yake Jongoo. Mama Jongoo akamuuliza, “Umemwona mwanangu?” Kuku hakujibu kitu. Mama Jongoo akapatwa na wasiwasi.

鸡回家的路上,遇到了千足虫妈妈。千足虫妈妈问它:“你看见我的孩子了吗?”鸡什么都没说,千足虫妈妈很担心。


Mama Jongoo akasikia sauti kwa mbali. “Nisaidie mama!” ile sauti ililia. Mama Jongoo akaangalia huku na kule na kusikiliza kwa makini. Sauti ilitokea tumboni mwa kuku.

千足虫妈妈突然听到了一阵微弱的声音:“快帮我,妈妈!”千足虫妈妈看了看周围,仔细地听着,声音是从鸡身体里传出来的。


Mama Jongoo alipiga kelele, “Tumia nguvu yako ya kipekee mwanangu!” Majongoo wanaweza kutoa harufu mbaya na ladha ya ajabu. Kuku akaanza kujisikia mgonjwa.

千足虫妈妈大喊道:“快用你神奇的能力!”千足虫会产生一种很难闻的味道,会让鸡觉得很恶心。


Kuku akabeuwa. Akameza mate na kutema. Halafu akapiga chafya na kukohoa. Akakohoa tena. Jongoo alimfanya ajisikie vibaya.

鸡打了一个嗝,咕噜咕噜要吐了,又是打喷嚏又是咳嗽。千足虫太恶心了!


Kuku alikohoa, hadi akamtema jongoo aliyekuwa tumboni mwake. Mama Jongoo na mwanaye wakakwea mti kujificha.

鸡不停地咳嗽,直到把千足虫从胃里咳了出来。千足虫妈妈和孩子赶紧爬上树,藏了起来。


Tangu hapo, Kuku na Jongoo ni maadui.

从此以后,鸡和千足虫就变成了敌人。


作者: Winny Asara
插图: Magriet Brink
译文: Matteo E. Mwita
配音: Lauwo George
语言: 斯瓦希里语
级别: 3级
出处: 原文来自非洲故事书Chicken and Millipede
共享创意授权条款
本着作系采用共享创意 署名 3.0 未本地化版本授权条款授权。
选项
返回故事列表 下载 PDF