Kuku na Jongoo walikuwa marafiki. Ila walikuwa wanashindana kila mara. Siku moja wakaamua kucheza mpira wa miguu ili waweze kubaini nani alikuwa mchezaji bora zaidi.
鸡和千足虫是好朋友,但是它们又互相竞争。有一天,它们决定进行一场足球比赛,看看谁是最棒的球员。
Wakaenda uwanjani na wakaanza kucheza. Kuku alikuwa na kasi ila Jongoo alikuwa na kasi zaidi. Kuku alipiga mpira mbali, ila Jongoo alipiga mbali zaidi. Kuku akaanza kupandwa na hasira.
Kuku akakasirika kwa kuwa amefungwa. Hakuwa mshindani mzuri. Jongoo akaanza kucheka kwa sababu rafiki yake alikuwa analalamika.
鸡输了,它很生气。千足虫哈哈大笑,因为它的朋友输了球,就无理取闹。
Kuku alipatwa na hasira kiasi kwamba akafungua mdomo wake mkubwa na akammeza Jongoo.
鸡生气极了,它张开嘴,一口把千足虫吞了下去。
Kuku alipokuwa anarudi nyumbani alikutana na Mama yake Jongoo. Mama Jongoo akamuuliza, “Umemwona mwanangu?” Kuku hakujibu kitu. Mama Jongoo akapatwa na wasiwasi.
Mama Jongoo akasikia sauti kwa mbali. “Nisaidie mama!” ile sauti ililia. Mama Jongoo akaangalia huku na kule na kusikiliza kwa makini. Sauti ilitokea tumboni mwa kuku.
Mama Jongoo alipiga kelele, “Tumia nguvu yako ya kipekee mwanangu!” Majongoo wanaweza kutoa harufu mbaya na ladha ya ajabu. Kuku akaanza kujisikia mgonjwa.
千足虫妈妈大喊道:“快用你神奇的能力!”千足虫会产生一种很难闻的味道,会让鸡觉得很恶心。
Kuku akabeuwa. Akameza mate na kutema. Halafu akapiga chafya na kukohoa. Akakohoa tena. Jongoo alimfanya ajisikie vibaya.
鸡打了一个嗝,咕噜咕噜要吐了,又是打喷嚏又是咳嗽。千足虫太恶心了!
Kuku alikohoa, hadi akamtema jongoo aliyekuwa tumboni mwake. Mama Jongoo na mwanaye wakakwea mti kujificha.