تحميل بصيغة PDF
العودة لقائمة القصص

Mtoto Punda صغير الحمار

كُتِب بواسطة Lindiwe Matshikiza

رسمة بواسطة Meghan Judge

بترجمة Monica Shank Lauwo, Lauwo George

قرأه Lauwo George

لغة السواحلية

مستوى المستوى 3

سرد للقصة كاملة

سرعة القراءة

تشغيل تلقائي للقصة


Ilikuwa ni msichana mdogo aliyekuwa wa kwanza kuona umbo la ajabu kwa mbali.

كانت الفتاة الصغيرة هي أول من رأى الشبح الغامض قادماً من بعيد.


Kadiri umbo lilipokaribia, aliona kwamba lilikuwa ni mwanamke mwenye ujauzito mkubwa.

وباقتراب الشكل الغامض منها، تبينت الفتاة بأنه شبح امرأة حامل.


Kwa upole na ujasiri, msichana alimsogelea mwanamke yule. “Lazima tumhifadhi,” watu wa msichana yule walisema. “Tutawaweka yeye na mtoto wake salama.”

تقدمت الفتاة نحو المرأة واقتربت منها، ببعض الخجل لكن بكل شجاعة. قال أهل الفتاة:” علينا أن نحتفظ بهذه المرأة بيننا. سوف نقوم بحمايتها هي وصغيرها”.


Mtoto alikuwa njiani kuzaliwa si muda mrefu. “Sukuma!” “Leteni mablanketi!” “Maji!” “Suuukuuumaaaa!!!”

وبعد مدة وجيزة حان موعد ولادة الصغير. قالت نساء القرية: “هيا ادفعي … هات الغطاء … هات الماء … ادفعيييييييي …”.


Lakini walipomwona mtoto, wote waliruka kwa mshtuko. “Punda?!”

لكن، وعندما رأت النسوة المولود قفزن إلى الوراء من هول الصدمة “حمار!”


Wakaanza kubishana. “Tulisema tutawaweka mama na mtoto salama, na hivyo ndivyo tutakavyofanya,” baadhi wakasema. “Lakini watatuletea mkosi!” wengine wakadai.

بدأت النسوة يتجادلن حول المولود الجديد. البعض قلن بأنهن سوف يحتفظن بالمولود وأمه لأنهن وعدنها بذلك، بينما تخوف البعض الأخر من أنهما قد يكونا نذير شؤم على القرية.


Kwa hiyo mwanamke yule alijikuta yuko peke yake kwa mara nyingine tena. Akajiuliza atafanya nini na mtoto huyo wa ajabu. Akajiuliza atafanya nini na yeye mwenyewe.

وهكذا وجدت المرأة نفسها وحيدة من جديد، تسأل نفسها في حيرة عما يمكن أن تفعله بهذا الطفل الأخرق وبنفسها.


Lakini hatimaye alikubali kwamba huyo ni mwanaye na yeye ni mama yake.

وانتهى بها التفكير إلى قبول الأمر، فهذا الحمار ابنها وهي الآن أمه.


Endapo mtoto huyo angebaki kuwa vilevile, na umbo dogo, labda kila kitu kingekuwa tofauti. Lakini mtoto Punda aliendelea kukua na kukua mpaka hakuweza kutoshea tena mgongoni mwa mama yake. Pamoja na kujaribu kwa bidii, hakuweza kuwa na tabia za kibinadamu. Mara nyingi mama yake alichoka na kuvunjika moyo. Wakati mwingine alimlazimisha kufanya kazi walizostahili wanyama.

ولو أن الجحش حافظ على حجمه الصغير لاختلف الأمر. لكن الجحش بدأ يكبر ويكبر حتى لم يعد بإمكان الأم حمله على ظهرها. وكان غير قادر على أن يسلك سلوك الآدميين مهما فعل ومهما حاول ذلك. أحست الأم بالتعب والإحباط، وكانت تكلفه أحيانا بأعمال يقوم بها الحيوانات.


Kuchanganyikiwa na hasira vilianza kujengeka ndani mwa Punda. Alishindwa kufanya hivi wala vile. Alishindwa kuwa hivi wala vile. Alipatwa na hasira sana kiasi kwamba, siku moja, alimpiga teke mama yake mpaka akaanguka chini.

نما بداخل الحمار شعور بالغضب والارتباك. إذ هو لا يعرف ما يفعله ولا من يكون ولا كيف يكون. وفي يوم من الأيام، بلغ الغضب بالحمار منتهاه لدرجة انه ركل أمَّه وأوقعها أرضا.


Punda alijawa na aibu. Akaanza kukimbilia mbali kwa haraka kadiri awezavyo.

شعر الحمار بعدها بالخجل الشديد لما بدر منه في حق أمه وانبرى هارباً بعيداً.


Wakati aliposimama, ilikuwa ni usiku, na alikuwa amepotea. “Hii hoo?” alinong’ona gizani. “Hii hoo?” giza likatoa mwangwi. Alikuwa mwenyewe. Alijikunyata katika umbo dogo, akalala fofofo usingizi wa mang’amung’amu.

ولما توقف عن الجري، كان الظلام قد أرخى سدوله على المكان فإذا بالحمار يضيع طريقه وإذا به يهمس للظلام: “هييه … هاو؟” ويردد رجع الصدى: “هييه … هاو؟”. وجد الحمار نفسه وحيدا فتكوم على نفسه وخلد إلى نوم عميق مضطرب.


Punda aliamka na kumkuta mzee mmoja wa ajabu akimtazama. Akamwangalia mzee yule machoni na akaanza kuhisi ishara ya matumaini.

وعندما استفاق من نومه، وجد شيخاً غريباً واقفاً عند رأسه محدقاً فيه. نظر الحمار في عيني الشيخ وبدأ يشعر ببصيص من الأمل.


Punda alienda kuishi na mzee yule, na mzee alimfundisha mbinu nyingi za kuishi. Punda alisikiliza na kujifunza, na mzee vivyo hivyo pia. Walisaidiana na kucheka pamoja.

انتقل الحمار للعيش مع الشيخ، فعلمه أساليب عديدة للعيش. استمع الاثنان إلى بعضهما وتعلما الكثير من بعضهما وتعاونا وضحكا كثيرا معا.


Asubuhi moja, mzee alimwomba Punda ambebe hadi kwenye kilele cha mlima.

وفي صباح أحد الأيام، طلب الشيخ من الحمار أن يحمله إلى قمة الجبل.


Walipofika juu kwenye mawingu, walipatwa na usingizi. Punda akaota kuwa mama yake alikuwa mgonjwa na alimhitaji. Na alipoamka…

وهناك بين السحب، خلد الاثنان إلى النوم. حلم الحمار بأن أمه مريضة وبأنها تناديه. وعندما استفاق من نومه،


…mawingu yalikuwa yametoweka pamoja na rafiki yake, yule mzee.

وجد الغيوم قد اختفت، وكذا صديقه الشيخ.


Hatimaye, Punda alijua alichotakiwa kufanya.

عندها، عرف الحمار ما يجب عليه فعله.


Punda alimkuta mama yake akiwa peke yake huku akimwomboleza mwanaye aliyepotea. Wakaangaliana kwa muda mrefu. Na kisha wakakumbatiana kwa hisia.

ولدى رجوعه إلى البيت وجد أمه وحيدة ترثي ابنها المفقود. حدق الاثنان في بعضهما لفترة طويلة ثم عانق كل منهما الآخر عناقا حارا.


Mtoto Punda na mama yake wamekuwa kitu kimoja na kuishi kwa ushirikiano. Taratibu, familia nyingine zimeanza kuhamia na kuishi miongoni mwao.

كبر الحمار وأمه معاً ووجدا لنفسيهما سبلاً عديدة للتعايش في سلام جنباً إلى جنب. وشيئاً فشيئاً، بدأت عائلات أخرى تستقر حول الحمار وأمه.


كُتِب بواسطة: Lindiwe Matshikiza
رسمة بواسطة: Meghan Judge
بترجمة: Monica Shank Lauwo, Lauwo George
قرأه: Lauwo George
لغة: السواحلية
مستوى: المستوى 3
المصدر: Donkey Child از القصص الأفريقية القصيرة
رخصة المشاع الإبداعي
تحت مجوز المشاع الإبداعي نَسب المُصنَّف 4.0 دولي کریتز کامنز به نشر رسید.
خيارات
العودة لقائمة القصص تحميل بصيغة PDF